Makabiliano yanaendelea kati ya makundi ya waasi kutoka jimbo la Puntland nchini Somalia kuchukua uthibiti wa mji na bandari ya Kismayo. Kundi linaloongozwa na Ahmed Madobe aliyejitangaza rais wa eneo hilo limeimarisha ulinzi wake katika mji huo baada ya makabiliano kuzuka siku ya Ijumaa wiki iliyopita.
Waasi hao wa Ras Kamboni wanasema kuwa eneo hilo ni muhimu sana kwa uchumi wake na ni sharti liwe chini ya ulinzi wao baada ya Al-Shabab kukimbia. Mji wa Kismayo awali ulikuwa ngome ya wanamgambo wa Al-Shabab ambao walifurushwa na wanajeshi wa Kenya chini ya mwavuli wa majeshi ya Afrika AMISOM mwaka uliopita.
Wachambuzi wa siasa za Somalia wanasema kuwa mji wa Kismayo ni muhimu sana kwa uchumi wa jimbo la Jubaland ambalo linapatikana na Kenya na Ethiopia na kutambuliwa na serikali ya Mogadishu. Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud, anasema makundi haya ya waasi kutoka Jubaland na Puntland wanaokabiliana kuchukua uthibiti wa mji wa Kismayo wanastahili kuacha mapigano na kuungana kuendeleza maeneo yao. Wiki iliyopita, marais wa Kenya na Somalia walikutana jijini Nairobi kuzungumzia hali ya usalama katika jimbo hilo la Jubaland ambalo linafahamika mno kwa biashara ya mkaa na kuwa utajiri wa ardhi yenye rutuba pamoja na midogi ya gesi.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO