Friday, June 14, 2013

SAUDIA YAWATIA MBARONI WAANDAMANAJI 150

Vikosi vya usalama vya ukoo wa kifalme wa Saudi Arabia vimewatia mbaroni karibu waandamanaji 150 walioshiriki katika maandamano kwenye miji mbalimbali wakitaka kuachiliwa huru wafungwa wa kisiasa.
Waandamanaji hao waliandamana licha ya ukoo wa kifalme wa Saudia kupiga marufuku maandamano dhidi ya serikali. Tangu mwanzoni mwa mwaka 2011 nchi hiyo imekuwa ikishuhudia maandamano huku makumi ya waandamanaji wakiuawa na wengine wengi kutiwa mbaroni.
Wanaharakati wa haki za binadamu nchini Saudia wamelaani ukandamizaji unaofanywa na vikosi vya usalama vya ukoo wa kifalme nchini humo na kusema kuwa, kuna zaidi ya wafungwa 40,000 wa kisiasa wanaoshikiliwa katika jela mbali mbali za Saudia.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO