Friday, June 14, 2013

UINGEREZA YAKATAA KUIUZIA SILAHA ISRAEL

Gazeti la Kizayuni Haaretz linalochapishwa huko Israel limeandika kuwa, Uingereza imekataa mara kadhaa kuiuzia silaha na zana za kijeshi utawala wa Kizayuni wa Israel kwa hofu kwamba zitatumika dhidi ya wananchi wa Palestina au wapinzani walioko ndani ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu. Gazeti hilo limefichua kuwa, tokea mwaka 2008 hadi 2012, utawala wa Kizayuni wa Israel umetuma maombi 52 ya kununua silaha na zana za kivita kutoka Uingereza, lakini serikali ya London imekataa kutekeleza maombi ya Tel Aviv. Gazeti hilo limeandika kuwa, miongoni mwa zana za kijeshi zilizoombwa na Israel ni boti za mwendo wa kasi, mizinga, zana za mawasiliano ya kijeshi, vipuri vya helkopta na ndege za kivita, mfumo wa kuongozea ndege, fulana za kuzuia risasi, rada za angani na mada za kemikali. Gazeti hilo limeandika kuwa, licha ya Uingereza, Uholanzi nayo pia imekataa kuiuzia silaha na zana za kijeshi  utawala wa Kizayuni wa Israel, kwa hofu kwamba silaha hizo zitatumika dhidi ya wananchi wa Palestina.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO