Tuesday, June 11, 2013

WAZIRI MKUU WA UTURUKI KUKUTANA NA WAANDAMAJI

Polisi wa kupambana na ghasia wanapiga kambi jijini Istabul kukabiliana na waandamanaji wanaoipinga serikali ya Waziri Mkuu Recep Tayyip Erdogan. Maandamano hayo yamekuwa yakiendelea kwa wiki mbili sasa na polisi wamekuwa wakitumia mabomu ya kutoa machozi kuwasambaratisha wapinzani hao bila mafanikio.Waziri Mkuu Erdogan amekubali kukutana na waandamnaji hao siku ya Jumatano kusikia kilio chao.
Mwishoni mwa juma lililopita, Waziri Mkuu Erdogan aliwaambia wafuasi wake kuwa wamekuwa wavumilivu mno na mwishoni mwa wiki hii nao wataanza mikutano yao ya hadhara na maadamano kuwapinga wale wanaoandamana dhidi ya serikali. Maandamano nchini Uturuki yalianza mwisho mwa mwezi uliopita jijini Instabul na kusambaa kote nchini kupinga uongozi wa Erdogan ambao waandamanaji hao wanasema ni wa Kidikteta.
Waandamanaji zaidi ya 5,000 wamejeruhiwa kutokana na maandamano hayo wengi wao ambao ni vijana. Serikali imewaomba msahama wale wote waliojeruhuhiwa na kuwaambia kuachana na maandamano hayo. Waziri Mkuu Erdogan amewaambia waandamanaji hao kuwa atawapa somo kupitia uchaguzi wa Kidemokrasia nchini humo. Umoja wa Ulaya umetoa wito kwa serikali nchini humo kupata suluhu la kudumu kuhusu maandamano hayo.Watu watatu akiwemo mwanajeshi mmoja wameuawa .

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO