Ndege iliokuwa imembeba kiongozi aliyena itikadi kali za kiislamu Abu Qatada imeondoka hii leo kutoka Uingereza ikielekea nchini Jordan. Hii ni Kulingana na mpiga picha wa shirika la habari la AFP. Hatua ya kumuondoa Abu Qatada nchini Uingereza imemaliza vuta nikuvute ya takriban muongo mmoja ya kutaka kumrudisha kwao.
Picha za Televisheni zilimuonesha Abu Qatada kiongozi aliyezaliwa Palestina akiwa amevalia kanzu nyeupe akiingia katika ndege hiyo Magharibi mwa London.
Waziri wa maswala ya kijamii nchini Uingereza Theresa May amethibitisha kuondoka kwa kiongozi huyo aliye na umri wa miaka 53 na aliyeaminika kuwa na mafungamano na Osama Bin Laden. May amesema Abu Qatada amerudishwa nchini Jordan ili ajibu mashtaka ya ugaidi yanayomkabili.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO