Tuesday, July 09, 2013

BLAIR ATAKA SYRIA IINGILIWE KIJESHI

Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair ametaka kutumwa majeshi ya kigeni nchini Syria pamoja na kuwekwa eneo la marufuku kupaa ndege nchini humo.
Blair ameikosoa vikali serikali ya London kwa kusitasita kuchukua maamuzi ya kuwatumia silaha magaidi wa Syria. Tony Blair ambaye ni mwakilishi maalumu wa kundi la pande nne la amani katika Mashariki ya Kati linaloundwa na  Marekani, Russia, Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya na ambaye alipaswa kuchukua msimamo usioegemea upande wowote katika mgogoro wa Syria, amesema kuwa, wapinzani nchini humo hawatafanikiwa iwapo majeshi ya kigeni hayatatumwa huko Syria.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, mwaka 2003 Blair akishirikiana na George W. Bush Rais wa zamani wa Marekani walianzisha mashambulio ya kijeshi dhidi ya Iraq kwa kisingizio kwamba nchi hiyo inamiliki silaha za mauaji ya halaiki, madai ambayo hadi leo bado hayajathibitishwa na Washington wala London.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO