Tuesday, July 09, 2013

WAFUASI WA UDUGU WA KIISLAM 53 WAUAWA MISRI

Harakati ya Ikhwanul Muslimin ya Misri imesema kuwa idadi ya watu waliouawa katika mashambulizi ya leo ya jeshi la nchi hiyo dhidi ya wafuasi wa Muhammad Morsi, rais wa nchi iyo aliyepinduliwa na jeshi imeongezeka na kufikia watu 53 wakiwemo watoto watano.
Ikhwanul Muslimin imesema kuwa, wafuasi wake wameuawa wakati jeshi la Misri lilipoushambulia umati wa watu hao waliokuwa wameketi chini nje ya kambi zao wakipinga kitendo cha kupinduliwa Rais Muhammad Morsi.
Wizara ya Afya ya Misri imetaja idadi ya waliouawa kwenye mashambulizi hayo ya jeshi ya leo kuwa watu 40. Watu walioshuhudia wameeleza kuwa jeshi la Misri limetumia silaha hai kuwatawanya wafuasi wa Muhammad Morsi huko katika mji wa Nasr mashariki mwa Cairo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO