Kundi la Upinzani la Iran lililo uhamishoni limedai kuwa lina ushahidi juu ya kuwepo kwa vinu vya Nuklia vinavyodaiwa kuwa katika mji wa Damavand kaskazini mashariki mwa Tehran. Kundi hilo la wanamgambo wa kijahidina la nchini Iran (MEK) lililo na makazi yake jijini Paris nchini Ufaransa limesema kuwa Vinu hivyo vimekuwepo nchini humo tangu mwaka 2006. Kundi la MEK liliundwa mwaka 1960 kupinga utawala wa kifalme lilionekana na Marekani kuwa la Kigaidi mpaka mwaka jana, ambapo mara kadhaa lilitoa Taarifa juu ya mpango wa Nuklia wa Iran. Chama hicho kimeelezwa kuwa na ushahidi wa kuaminika juu Vinu vya siri vya Iran ushahidi ambao ulikusanywa kwa kipindi cha mwaka mmoja kutoka kwa vyanzo 50 vya taarifa hizo vikiwemo vya ndani ya utawala wa Iran.
Mradi huo wa siri unadaiwa kufanya chini ya ardhi chini ya mlima karibu na mji wa Damavand, huku MEK imedai kuwa wanahisi kuwa Mradi huu mpya wa Nuklia unalenga kutengeneza silaha za kibiolojia na Kemikali. Ripoti hiyo imesema ugunduzi huu unaonesha kwa mara nyingine kuwa Utawala wa Mullah hauna dhamira yeyota ya kusitisha au kuacha kabisa mpango wa utengenezaji wa silaha za Nuklia.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO