Mwanaharakati wa nchini Pakistani Malala Yousafzai amewasili ndani ya Umoja wa Mataifa hii leo, ikiwa ni miezi tisa baada ya kushambuliwa kwa risasi kichwani na kundi la Wanamgambo wa Taliban wakiamini kuwa watamaliza Kampeni za binti huyo juu ya kupigania Wasichana kupatiwa haki ya Elimu. Binti huyo atatimiza umri wa miaka 16 Wakati huu akitarajiwa kutoa hotuba ya kwanza hadharani tangu aliponusurika kifo kutokana na Shambulio kwenye basi la Shule karibu na nyumbani kwake nchini Pakistani. Malala amekuwa Binti wa mfano duniani kote na kuwa Mshindi mdogo wa Tuzo la Nobel ambaye hakuwahi kutokea na kuripotiwa na vyombo vya habari kuwa miongoni mwa Watu Maarufu kwa mwaka 2013.
Binti huyu amekuwa mfano mkubwa si tu kwa ajili ya kupigania haki ya Wasichana kupata Elimu, lakini pia kwa wito wake wa kutaka jumuia ya Kimataifa kutafuta suluhu swala hili haraka iwezekanavyo, mjimbe wa Umoja wa Mataifa wa maswala ya Elimu ameeleza. Malala anatarajiwa kuhutubia Mkutano wa Vijana wa Umoja wa Mataifa, kutoa ujumbe kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon na Viongozi wengine duniani juu ya uhitaji wa kutimiza ahadi ya Kuhakikisha malengo ya Milenia ya elimu kwa Wasichana inatimia ifikapo mwaka 2015. Pia atawasilisha Ombi kwa Ban Ki Moon lililotiwa saini na Watu zaidi ya 330,000 wakitaka nchi Wanachama 193 wa Umoja wa Mataifa kuwasaidia kifedha Walimu, Shule na Vitabu kwa ajili ya kutimiza lengo.
Wanamgambo wa Taliban walisema Shambulio dhidi ya Malala lililenga kufikisha ujumbe kwa Dunia kuwa Wasichana hawana haki ya kupata elimu. Hata hivyo hizi sasa Wasichana wengi zaidi wameanza kwenda Shule kupata elimu. Umoja wa Mataifa umeripoti kuwa Watoto takriban Milioni 57 wanaopaswa kuanza elimu ya msingi hawapati elimu hiyo, nusu ya Idadi hiyo ni kwa nchi zilizo na migogoro kama Syria.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO