Korea Kaskazini imesema haitaangamiza silaha zake za nyuklia hadi pale Marekani itakapositisha sera za uhasama dhidi yake. Balozi wa Korea Kaskazini katika Umoja wa Mataifa So Se Pyong ameyasema hayo mjini Geneva na kuongeza kuwa kikosi cha jeshi la Umoja wa Mataifa kinachosimamiwa na Marekani huko Korea Kusini kinapaswa pia kuvunjwa kwani kinatumiwa kueneza uhasama dhidi ya Pyongyang.
Balozi huyo hata hivyo amesema Korea Kaskazini iko tayari kurejea katika meza ya mazunguzmo ya nyuklia yaliyositishwa mwaka 2008.
Aidha ameonya kuhusu mazoezi yajayo ya pamoja ya kijeshi baina ya Marekani na Korea Kusini na kusema luteka hiyo itaongeza hali ya wasi wasi katika Peninsula ya Korea.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO