Thursday, July 11, 2013

WAARABU WATAKA ISRAEL IJIUNGE NA NPT

Wanadiplomasia wa nchi za Kiarabu wanakusudia kuwasilisha rasmi malalamiko yao kwenye kikao kijacho cha Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia (IAEA), na kuutaka wakala huo kusimamia kikamilifu mitambo ya nyuklia ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
Taarifa zinasema kuwa, nchi za Kiarabu zinakasirishwa na hatua ya kutofungamana utawala huo ghasibu na mpango wa kuanzishwa eneo la Mashariki ya Kati bila ya  silaha za nyuklia. Taarifa zinasema kuwa, nchi 18 za Kiarabu zilizoko kwenye wakala wa IAEA zimemtaka Mkurugenzi Mkuu wa IAEA Yukiya Amano alijadili kwa kina suala la umiliki silaha za nyuklia utawala wa Israel kwenye kikao kijacho kitakachoanza tarehe 16 hadi 20 mwezi Septemba mwaka huu. Taarifa hiyo inaeleza kuwa, utawala wa Israel unapaswa kuweka wazi shughuli zake za nyuklia kwa wakala wa IAEA na kuutaka utawala huo utie saini makubaliano ya kuzuia uzalishaji, utumiaji na usambazaji wa silaha za nyuklia NPT. Duru za habari zinasema kuwa, mkakati huo wa nchi za Kiarabu utakabiliwa na upinzani mkubwa wa Marekani na waitifaki wake wa Ulaya.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO