Mafuriko yanayotokea katika maeneo ya milima ya Himalaya magharibi mwa China yameharibu madaraja , nyumba na kusababisha maporomoko ya ardhi , na watu 19 wanahofiwa kuwa wamefariki na wengine kadha hawajulikani waliko, wakati mvua kubwa zinanyesha katika maeneo kadha ya nchi hiyo. Mafuriko katika jimbo la magharibi la Sichuan ni mabaya kabisa katika muda wa miaka 50 iliyopita katika baadhi ya maeneo, wakati zaidi ya watu 100,000 wamelazimika kuyahama makaazi yao.
Kwa mujibu wa wizara ya masuala ya jamii nchini humo , kiasi ya watu wapatao milioni 1.6 wameathirika tangu Jumapili iliyopita na nyumba elfu kadha zimeharibiwa.
Kiasi ya watu 100 wamekufa ama hawajulikani waliko. Wengi waliofariki katika jimbo la Sichuan ni kutokana na maporomoko makubwa ya ardhi ambayo yametokea katika eneo la kitalii nje ya mji wa Dujiangyan.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO