Sunday, February 03, 2013

MPANGO WA BIDDEN KUTATUA MZOZO WA NYUKLIA WA IRAN


Rais Barack Obama wa Marekani amesisitiza katika duru yake ya pili ya urais nchini humo juu ya udiplomasia wa "mashinikizo na vikwazo" na amempa makamu wake Jo Biden jukumu la kufuatilia kadhia ya nyuklia ya Iran. Biden ambaye ameelekea Munich, Ujerumani kwa ajili ya kushiriki katika kikao cha usalama, ameeleza kuwa nchi yake iko tayari kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na Iran na kwamba Washington ina mpango ambao kwa mujibu wa madai yake unaweza ukafungua njia ya kutatuliwa kidiplomasia kadhia ya nyuklia ya Iran. Biden amesema pia kuwa Marekani haitairuhusu Iran kumiliki silaha za nyuklia na kwamba mlango wa mazungumzo ya amani na Tehran hautakuwa wazi milele. 
Matamshi hayo ya Joe Biden yamekaribishwa na kuungwa mkono na viongozi wa Umoja wa Ulaya akiwemo Catherine Ashton, Mkuu wa Siasa za Nje wa umoja huo na Guido Westewelle, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani. Matamshi ya kiongozi huyo wa White House yanaonesha kwamba Marekani inaendeleza siasa zake za propaganda chafu dhidi ya Iran na kwamba Tehran kwa mujibu wa mtazamo wa Wamagharibi, ni mtuhumiwa mkubwa; kwa sababu hiyo mazungumzo ya aina yoyote ile na Iran yanapaswa kufanyika kwa mujibu wa madai hayo yasiyo na msingi. Kwa hakika hatua hiyo ya Marekani ina lengo la kuidhihirisha serikali ya Washington kuwa ina nia njema ya kutaka kutatua kadhia ya nyuklia ya Iran kwa njia za kidiplomasia.
Ukweli wa mambo ni kuwa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel zimepanga njama kabambe na harakati kubwa kwa ajili ya kikao cha Munich na zinafanya juhudi ili kunufaika na fursa hiyo dhidi ya miradi ya kuzalisha nishati ya nyuklia ya Iran. Ni kwa sababu hiyo ndio maana katika hotuba yake kwenye mkutano wa Munich, Makamu wa Rais wa Marekani amefanya jitihada kubwa za kuchafua sura ya Iran badala ya kuzungumzia haki za nyuklia za Jamhuri ya Kiislamu.   Hii ni katika hali ambayo viongozi wa Iran wamekosoa vikali suala la kubadilishwa mahali na tarehe ya kufanyika mazungumzo kati ya Tehran na kundi la 5+1 na hatua ya nchi za Magharibi ya kuchapisha habari za uwongo kuhusiana na suala hilo. Tangu karibu miezi 8 iliyopita yaani tangu baada ya kikao cha Moscow, Iran ilikuwa imejiandaa kufanya duru mpya ya mazungumzo, lakini upande wa Magharibi umekataa kuketi kwenye meza ya mazungumzo kwa sababu ambazo Iran pia haizijui.
Suala kuu hapa si wakati wa kufanyika mazungumzo hayo wala mahala gani yatafanyika, bali ni jambo jingine ambalo ni kuwa, baadhi ya wanachama wa kundi la 5+1 hawako tayari kufanya mazungumzo hayo. Viongozi wa Marekani wameelewa kuwa Russia na China hazichezi tena katika uwanja wa udiplomasia wa Magharibi kama ilivyokuwa huko nyuma na migongano ya mitazamo ya Kremlin na Peking na ile ya Marekani imepanuka na kugusa masuala mengi kuanzia mgogoro wa Syria hadi kadhia ya nyuklia ya Iran. Kwa sababu hiyo maafisa wa serikali ya Marekani wametoa fikra ya kufanyika mazungumzo ya moja kwa moja na Iran. Hatua hiyo imechukuliwa kwa sababu kadhaa. Kwanza ni kuwa Marekani na baadhi ya waitifaki wake wa Ulaya walitarajia kuwa vikwazo vyao dhidi ya Iran vitazusha uasi na machafuko ya kijamii. Hata hivyo badala ya kuwafanya wananchi wa Iran waichukie serikali na mfumo wao, vikwazo hivyo vimewafanya wazichukie zaidi nchi za Magharibi.
Sababu ya pili ni kuwa tofauti na makelele yake ya kipropaganda, Marekani haijaweza kubuni stratijia ya maana kwa ajili ya kuanza mazungumzo na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Hii ni kwa sababu tunapotazama mwenendo wa Marekani kuhusu Iran tutatambua kuwa madai ya kutaka kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na Tehran hayana maana yoyote. Ukweli ni kuwa lengo la Marekani katika harakati yake hiyo ni kutaka kubadili mlingano wa kimataifa kuhusu suala la mazungumzo na Iran. Duru za kisiasa za nchi za Magharibi pia zinatumia propaganda za vyombo vya habari kuonesha kuwa Iran haiko tayari kufanya mazungumzo na kwa njia hiyo itambulike kuwa ni tishio kwa jamii ya kimataifa.      

IRAN INA HAKI YA KUTUMIA NYUKLIA


Serikali ya China imesisitiza kwamba, Iran ina haki kamili ya kunufaika na teknolojia ya kisasa ya nishati ya nyuklia kwa matumizi ya amani. Hong Lei, Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya China amesema kuwa, daima Beijing imekuwa ikiunga mkono ushirikiano wa Tehran na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA). Amesema, China inaamini kwamba, mazungumzo na ushirikiano ndio njia pekee na sahihi ya kuondoa suutafahumu kuhusiana na suala la miradi ya nyuklia ya Iran na imekuwa ikizishajiisha pande mbili hizo kushirikiana zaidi. Msemaji huyo wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya China ameongeza kuwa, Iran ikiwa miongoni mwa nchi zilizotia saini Mkataba wa Kuzuia Uzalishaji na Usambazaji wa Silaha za Nyuklia NPT ina haki ya kustafidi na teknolojia ya nyuklia kwa matumizi ya amani. Licha ya kuwa miradi ya nyuklia ya Iran ni kwa ajili ya matumini ya amani na imekuwa ikifanyika chini ya usimamizi wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA, lakini Marekani, utawala wa Kizayuni wa Israel na waitifaki wao wamekuwa wakiituhumu Tehran kwamba, miradi yake ya nyuklia ni kwa ajili ya malengo ya kijeshi, tuhuma ambazo hazina msingi wowote.

WAFUNGWA WA KIISLAM UK WALAZIMISHWA KULA NGURUWE


Haki za Waislamu nchini Uingereza zimeendelea kukiukwa huku wafungwa wa Kiislamu wanaotumikia vifungo katika magereza ya nchi hiyo wakilazimishwa kula nyama ya nguruwe. Shirika moja la kutetea haki za binadamu limetangaza kuwa, serikali ya Uingereza imekuwa ikikiuka haki za wafungwa wa Kiislamu katika magereza ya nchi hiyo. Taarifa zaidi zinasema, serikali ya Uingereza imekataa kupeleka nyama halali kwa ajili ya wafungwa wa Kiislamu katika magereza ya nchi hiyo na badala yake imekuwa ikiwalazimisha wafungwa hao wa Kiislamu kula nyama ya nguruwe ambayo kwa mujibu wa mafundisho ya dini yao ni haramu. Imeelezwa kuwa, katika baadhi ya magereza wahusika katika magereza hayo wamekuwa wakipeleka nyama ya nguruwe na kupuuza kwamba, kuna wafungwa ambao ni wafuasi wa dini ya Kiislamu. Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, katika baadhi ya magereza nyama ya matumizi kwa ajili ya wafungwa imepatikana ikiwa imechanganywa na nyama ya nguruwe. Shirika linalotetea mageuzi katika magereza nchini Uingereza limetoa wito wa kufanyika uchunguzi kuhusiana na ukiukaji wa haki za binadamu katika magereza ya nchi hiyo.

NDUGU UPO OFFLINE MBONA KWA MUDA MREFU


????OFFLINE????

Itakuja siku watu wote watakuwa hawakuoni online bali utakuwa offline!...
Marafiki zako wa karibu watakuwa wakikusubiri kwa hamu,lakini huto weza ingia online?!...
Watakutumia barua ! lakini huto wajibu!...
Watakusubiri masaa mengi katika:
WhatsApps, Facebook,Twitter,Yahoo , hotmail,!?...
Lakini hali itakuwa ni vile vile tu, offline!!!...
Siku hiyo comments zako sitasimama!...
Kwa sababu utakuwa?.

#################

Ushaondoka katika dunia hii !!!....
Huto kuwa na uwezo wa kuingia online!...
Wala kujibu barua zetu!...
Wala kuweka comment ya aina yoyote!
Na wala huto kuwa na uwezo wa kusahihisha yale uliyo yaandika hapo kabla!
Wala kumtaka msamaha yule uliye mkosea!.....
Wakati huo huto kuwa nasi!!!.....

Wakati huo utakuwa upo

################

Katika shimo dogo lenye kubana na lenye kiza!!!.....
Utakuwa upo kaburini!!!!!.....
Peke yako!..
Hakuna hata mmoja katika jamaa zako ambao walikupenda sana???!!!!......
Unajuta juu ya matendo yako!.....
Au huenda ukawa unaliwazika juu ya matendo yako mema?..
Umetutoka???!!!!....
Haujatuachia isipokuwa yale yaliyo andikwa na mikono yako!...
Au comments zako,yale uliyo yaweka katika wall yako na katika profile lako!!!.....
???????.
Ndugu yangu mpendwa chunga sana juu ya yale unayo yaweka katika profile lako!!!..
Wall yako na comment zako!...
Ili yasije kuwa ni madhambi ambayo yanaendelea kukujia hali ya kuwa wewe upo kaburini?
Kwani kila binadamu ni mwenye kuhesabiwa juu ya yale anayo yatenda!...
Kwa hiyo kuanzia hivi sasa Mtubie Allah na badilisha profile lako?
Ondoa picha zisizo ridhiwa na Allah?
Kabla ya kututoka na kupelekwa Offline!!!
Pindi utakapo kuwa huna uwezo wa kubadilisha lolote .
******************************
Kama imekupendeza itume kwa wengine ili ukumbusho uweze wafikia waislamu wenzako.

TUELEKEZANE PEPONI
??????????

Tumia vyema muda wako usije kujutia ukiwa offline katika dunia hii.

Saturday, February 02, 2013

IRAN YAONYESHA NDEGE YAKE YA KIVITA QAHER-313


Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeonyesha ndege yake ya kivita iliyotengenezwa hapa nchini ambayo uwezo wake ni sawa na ndege ya kivita ya Marekani ya F/A 18. Ndege hiyo ya kivita yenye jina la Qaher-313 yaani mshindi imeonyeshwa katika marasimu yaliyofanyika leo Jumamosi na kuhudhuriwa na Meja Jenerali Ataollah Salehi Kamanda wa Jeshi la Iran, Waziri wa Ulinzi wa Iran Brigedia Jenerali Ahmad Vahidi na Kamanda wa Jeshi la Anga la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Brigedia Jenerali Hassan Shah Safi katika maadhimisho ya Alfajiri Kumi katika kukumbuka ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu mwaka 1979. 


Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran amesema katika ufunguzi wa sherehe hizo kuwa ndege hiyo ya kivita ya Iran imebuniwa na kutengenezwa kikamilifu na wataalamu wa Iran.


MALENGO YA NYUMA YA PAZIA YA W/MKUU WA UINGEREZA LIBYA


David Cameroon Waziri Mkuu wa Uingereza akishiriki kwenye mkutano wa waandishi wa habari pamoja na Ali Zidan Waziri Mkuu wa serikali ya mpito ya Libya mjini Tripoli amesema kuwa, serikali ya London iko tayari kutumia uwezo wake wote wa kijeshi  kwa shabaha ya kutoa mafunzo kwa wanajeshi na maafisa wa vikosi vya usalama vya Libya. Cameroon amebainisha kuwa lengo kuu la serikali ya Uingereza ni kuisaidia serikali ya Libya katika kuleta amani na uthabiti kamili nchini humo. Aidha amesisitiza kwamba, London iko tayari kusaidia ujenzi mpya na kuikarabati nchi hiyo iliyoharibiwa na vita. Waziri Mkuu wa Uingereza siku ya Alhamisi aliwasili nchini Libya bila ya kutolewa taarifa za awali. Duru ya pili ya uingiliaji kati wa Uingereza nchini Libya ambayo imetimia kwa kisingizio cha kusaidia ujenzi mpya,  imefanyika kwa madhumuni ya  kupora maliasili ya nchi hiyo  na hasa mafuta na gesi. Awali Uingereza ilijitumbukiza nchini humo kwa lengo la kuuondoa madarakani utawala wa dikteta Muammar Gaddafi.
Tunaweza kusema kuwa, safari za David Cameroon Waziri Mkuu wa Uingereza na ile ya Nicolas Sarkozy Rais wa zamani wa Ufaransa, zote zimefanyika kwa malengo hayohayo. Hivi sasa Libya iko katika kipindi cha kujikarabati na weledi wa masuala  ya kisiasa wanaeleza kuwa, safari za viongozi wa Ulaya nchini humo zinafanyika kwa lengo la kutia saini mikataba ya mabilioni ya dola ya kuijenga upya nchi hiyo na hali kadhalika kupora maliasili ya nchi hiyo yakiwemo mafuta. Amma swali ambalo hadi sasa bado halijapata jibu ni hili kwamba; je, ni kwa nini nchi za Magharibi katika opersheni zao za kijeshi katika kipindi cha miezi michache tu, zililenga na kuharibu kabisa miundombinu muhimu ya Libya vikiwemo viwanda vya kusafisha mafuta bila ya sababu zozote za kimsingi? Wataalamu wa masuala ya mafuta wanasema kuwa, visima vingi vya mafuta na gesi bado havijagunduliwa nchini humo. Amma maudhui nyingine ni suala la kuporwa mapinduzi ya Libya na nchi za Magharibi, katika hali ambayo, baadhi ya  wanamapinduzi walikuwa na matumaini  ya kuuangusha utawala wa  dikteta Gaddafi  kwa usaidizi tu wa nchini za Magharibi na wala si uingiliaji wao.
Hivi sasa nchi za Ulaya zikiongozwa na Ufaransa na Uingereza zinafuatilia kwa makini mabadiliko na matukio yanayoendelea  nchini Libya sanjari na kufanya  juhudi kubwa za kuishinikiza serikali ya Tripoli ishirikiane bega kwa bega na Wamagharibi. Kwa msingi huo, wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaeleza kuwa, lengo la safari za hivi karibuni za viongozi wa Uingereza na Ufaransa nchini Libya  ni kufanyika juhudi za kutaka kupora na kudhibiti utajiri wa nchi hiyo baada ya kuondoshwa utawala wa Gaddafi.  Swali la kiistratijia linaloulizwa hapa ni hili kwamba, je, Wamagharibi walikuwa  na mikakati gani kwa ajili ya wananchi wa Libya baada ya kuuangusha utawala wa Gaddafi, ghairi ya kupora maliasili na utajiri wa mafuta? Tokea wananchi wa Libya walipochukua  azma ya kuangusha utawala wa Gaddafi  na Wamagharibi nao  kujitumbukiza kwenye kadhia hiyo ,nchi hizo zimeingia kwenye awamu nyingine nayo ni kuongeza satua na ushawishi wao kwa wanamapinduzi ili ziweze kufikia malengo yao machafu. Wadadisi wa masuala ya kisiasa wanaeleza kuwa, mikakati mingine ya Wamagharibi nchini Libya ni kuudhofisha kadri iwezekanavyo Umoja wa Afrika, ambapo katika kadhia ya Libya umeshuhudiwa udhaifu mkubwa wa umoja huo katika kutatua mgogoro wa nchi hiyo. Kwa kutumia harakati zinazoendelea nchini Libya, Wamagharibi wataendelea kufanya juhudi za kuushinikiza  umoja huo ufanye kazi kwa maslahi yao.

WAZAYUNI WANADHIBITI VYOMBO VYA HABARI DUNIANI


Dakta Muhammad Sarafraz Mkuu wa Kitengo cha Matangazo ya Ng'ambo wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB amesema kuwa, mfumo wa Kizayuni unadhibiti kanali zote za habari ulimwenguni. Akizungumzia vita vipya dhidi ya vyombo vya kupasha habari vya Iran, Dakta Sarafraz amesema kuwa, iwapo itaanzishwa kanali ya habari itakayokuwa tofauti na kanali  nyinginezo, bila shaka  mfumo wa Kizayuni utaingilia kati na kuifuta kanali hiyo. Ameongeza kuwa, tarehe 28 Januari 2013 serikali ya Uhispania ilichukua maamuzi yanayokinzana wazi na uhuru wa kujieleza pale ilipotoa amri ya kukatwa matangazo ya kanali ya HispanTV ya Iran inayotangaza matangazo yake kwa lugha ya Kihispania. Dakta Sarafraz ameongeza kuwa, sehemu ya hisa ya shirika la huduma za satalaiti la Hispasat inafungamana na shirika la Eutelsat; na Mkurugenzi wa Eutelsat ni Mfaransa mweye asili ya Kizayuni ambaye hivi karibuni amekuwa akivisakama vyombo vya kupasha habari vya Iran huko Ulaya. Mkurugenzi wa Kitengo cha Matangazo ya Ng'ambo wa IRIB ameongeza kuwa, Marekani inajidai kuwa ni mtetezi mkubwa wa haki za binadamu, uhuru wa kujieleza na demokrasia, amma inawaunga mkono madikteta wa Bahrain na Saudia Arabia katika kuwakandamiza wananchi wa nchi hizo.

WANANCHI KUFANYA KAZI NI SIKU NNE, GAMBIA


Rais wa Gambia Yahya Jammeh ametoa amri kuwa wafanyikazi wote wa umma watafanya kazi siku nne pekee kwa wiki kuanzia leo Ijumaa . Ijumaa sasa itakuwa siku ya mapumziko sawa na Jumamosi na Jumapili.
Rais Jammeh anasema iwapo wananchi wa Gambia watafanya kazi siku nne kwa wiki watapata muda zaidi wa kusali, kushiriki maswala ya kijamii na kulima mashamba yao. Kwenye taarifa amesema wananchi wa Gambia wanapaswa kurejea mashambani na kupanda chakula na kuhakikisha wanakula chakula hicho ili taifa hilo liwe tajiri na lenye afya. Amesema kuwa mishahara yao haitapunguzwa kwa sababu kwa siku hizo nne watu watafanya kazi zaidi ya saa za kawaida ili kulipiza siku ya tano.
Shule za kitaifa hazitafunguliwa tena siku ya ijumaa.Sekta za kibinafsi zitafanya kazi hadi ijumaa lakini hazitaweza kufanya biashara yoyote na serikali siku hiyo. Rais Jammeh mwenye historia ya kuwa na tabia za kustaajabisha, hajawapa wananchi Gambia muda wa kujiandaa kwa mfumo huo mpya. Mwaka 2007 alitangaza kuwa anaweza kutibu ungonjwa wa Ukimwi kwa muda wa siku tatu akitumia mchanganyiko wa dawa za kienyeji. Tamko hilo lililaaniwa na wataalam wa matibabu kote duniani. Pia amekuwa akishtumiwa kwa ukiukaji wa haki za binadam. Mwaka jana wafungwa tisa waliokabiliwa na hukumu ya kifo walipigwa risasi na maafisa wa polisi huku rais Jammeh akiapa kuwaua wafungwa wote waliohukumiwa kifo katika muda wa wiki kadhaa. Baadaye alisimamisha mauaji hayo baada ya kukosolewa vikali na jamii ya kimataifa.

AI YALAANI UKIUKAJI HAKI ZA KIBINADAMU NCHINI MALI


Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International limelaani ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu yakiwemo mauaji ya watoto wadogo katika vita vya Ufaransa huko nchini Mali.
Taarifa ya Amnesty International imebainisha kwamba, ushahidi unaonesha kuwa, kuna kesi nyingi za ukiukaji wa haki za binadamu nchini Mali tangu Ufaransa ilipoanza kufanya mashambulio yake ya kijeshi kaskazini mwa nchi hiyo Januari 11 mwaka huu. Raia wa Mali wamekuwa wakiuawa kufuatia mashambulio ya anga ya Ufaransa na kesi ya karibuni kabisa ni kuuawa watoto watatu wa nchi hiyo.
Ripoti ya Amnesty International imetolewa baada ya kufanyika uchunguzi wa siku kumi huko Mali kuhusiana na hali ya haki za binadamu katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika. Taarifa hiyo imeongeza kuwa, uingiliaji wa kijeshi wa Ufaransa nchini Mali ulifanyika kwa kisingizio cha kukomesha mapigano katika nchi hiyo lakini kivitendo hali ya machafuko nchini humo imeshadidi.
Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International limelaani pia vitendo vya kuwanyonga raia vinavyofanywa na jeshi la Mali na kusisitiza kwamba, vitendo hivyo ni ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu na ukanyagaji wa sheria za kimataifa.

CLINTON: MAREKANI IMEPOTEZA HESHIMA KUISAIDIA ISRAEL


Waziri anayeondoka wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton amekiri kuwa Marekani haina hadhi na nafasi nzuri katika nchi za Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika.
Clinton ambaye alikuwa akizungumza katika kituo cha Baraza la Uhusiano wa Nje wa Marekani katika siku yake ya mwisho kama Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo amesema amekuwa akifuatilia fikra za waliowengi duniani na kwamba anapaswa kukiri kuwa katika muongo mmoja uliopita Marekani haikuwa na hadhi na nafasi nzuri katika nchi za Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika. Amesisitiza kuwa sababu ya suala hilo ni uungaji mkono mkubwa wa Marekani kwa utawala wa Israel.
Hillary Clinton pia amesema kuwa siasa za Marekani zimefeli katika ulimwengu wa Kiislamu. Hillary Clinton leo anakabidhi mikoba ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kwa John Kerry baada ya kuhudumu katika wizara hiyo tangu mwaka 2009.

JINAI ZA KIVITA ZA ISRAEL DHIDI YA PALESTINA


Wachunguzi wa haki za binaadamu katika Umoja wa Mataifa wameutaka utawala wa Israel kusitisha upanuzi wa vitongoji vya waloezi wa Kizayuni na kuwaondoa walowezi nusu milioni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Katika taarifa iliyotolewa Alkhamisi jopo la Umoja wa Mataifa limesema hatua ya kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina ni jambo ambalo linaweza kuhesabiwa kuwa jinai za kivita. Ripoti hiyo imeongeza kuwa ulowezi wa Wazayuni umechangia ukiukaji wa haki za Wapalestina kwa njia nyingi.
Bi. Christine Chanet aliyeoongoza jopo hilo amesema Israel inakiuka Mkataba wa Geneva kwa kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina. Baada ya kutolewa ripoti hiyo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa Israel inapaswa kusitisha harakati za ujenzi wa vitongoji katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ikiwa ni pamoja na Quds Mashariki. Mamlaka ya Ndani ya Palestina imetishia kuichukulia Israel hatua za kisheria katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) iwapo Tel Aviv itaendeleza ujenzi katika maeneo ya Palestina inayoyakaliwa kwa mabavu.

WAMAGHARIBI HAWATAKI KUUTATUA MGOGORO WA SYRIA


Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje wa Russia amesema kuwa, nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani zinazuia juhudi za Moscow za kuutatua mgogoro wa Syria kwa mujibu wa makubaliano ya Geneva. Alexander Lukashevich amesema kuwa, baadhi ya mikakati ya Russia yenye lengo la kukomesha mgogoro wa Syria imekuwa ikikabiliwa na upinzani mkubwa wa nchi za Magharibi na hasa Marekani.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje wa Russia ameongeza kuwa, Moscow inaamini kwamba kipindi hiki kinahitaji kuchukuliwa hatua madhubuti na za haraka zenye shabaha ya kukomesha machafuko nchini Syria, kwa kufunguliwa milango ya kufanyika mazungumzo. Lukashevich amesema kuwa, mgogoro wa Syria kamwe hauwezi kutatuliwa kwa njia ya mtutu wa bunduki.

LEBANON YAZITAKA NCHI ZA KIARABU KUCHUKUA HATUA DHIDI YA HUJUMA ZA ISRAEL SYRIA

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Lebanon, amezitaka nchi za Kiarabu kuchukua msimamo imara na madhubuti kuhusiana na mashambulio ya anga yaliyofanywa na ndege za utawala katili wa Kizayuni nchini Syria. Adenan Mansur ameyasema hayo hii leo katika radiamali ya kulaani vikali mashambulizi ya jioni ya jana ya utawala wa Kizayuni dhidi ya kituo cha utafiti wa sayansi cha Jamraya karibu na mji mkuu Damascus ambapo wafanyakazi wawili wa kituo hicho waliuawa na wengine watano kujeruhiwa. Amesema kuwa, nchi za Kiarabu zinatakiwa kuchukua msimamo imara dhidi ya hujuma hizo na kwamba, suala hilo ni la lazima. Mansur pia amesema, kwa mara kadhaa utawala haramu wa Kizayuni umekuwa ukitishia amani na usalama wa nchi za Kiarabu na kwamba, shambulio la Israel nchini Syria kwa mara nyingine linadhihirisha zaidi jinai na ukatili wa utawala huo haramu tangu ulipoasisiwa mnamo mwaka 1948 hadi leo. Tayari Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imetoa ripoti na kusema kuwa, iwapo habari hizo zitakuwa na ukweli basi hilo litahesabiwa kuwa ni shambulio la kichokozi dhidi ya nchi huru jambo ambalo linakiuka Hati ya Umoja wa Mataifa.

RAIS WA UFARANSA KUZURU MALI


Rais wa Ufaransa Francois Hollande anatarajiwa kuzuru Mali, ambako makabiliano ya wiki tatu kati ya waasi na wanajeshi yamekuwa yakiendelea. Wapiganaji hao walipata pigo kubwa kufuatia mashambulizi ya angani dhidi yao yaliyowalazimisha kutoroka. Aidha rais Holland atazuru Timbuktu,moja ya miji iliyokombolewa na wanajeshi wa Ufaransa wakishirikiana na wale wa Mali, Jumamosi wiki iliyopita.Bwana Hollande ataenda mjini Bamako kukutana na Rais wa Mpito Dioncounda Traore. Hatua ya jeshi la Ufaransa kuingilia hali nchini Mali, zimepelekea kukombolewa kwa sehemu kubwa ya Kaskazini mwa Mali iliyokuwa imetekwa na wapiganaji wa kiislamu.
Wanajeshi wa Ufaransa, kwa sasa wangali wanaendelea na harakati za kuukomboa kabisa mji wa Kidal, ambao ndio mji uliosalia chini ya wapiganaji wa kiisilamu walioanza harakati zao punde baada ya mapinduzi ya kijeshi kutokea nchini humo mwaka jana. Bwana Hollande ataambatana na mawaziri wake wa mambo ya kigeni Lauren Fabius, ulinzi Jean-Yves Le Drian na ustawi, Pascal Canin.
Awali waziri wa ulinzi, bwana Le Drian alisema kuwa wapiganaji walianza kutawanyika na hivyo kuashiria wakati muhimu katika msaada wa kijeshi wa wanjeshi wa Ufaransa. Kwa rais ambaye umaarufu wake ulikuwa umeanza kudidimia, anayekosolewa mara kwa mara kwa kukosa mwelekeo, hatua ya jeshi lake nchini Mali imepongezwa sana kulingana na mwandishi wa BB C mjini Paris Christian Fraser.
Ushawishi wa rais Hollande umeanza kuimarika kulingana na kura za maoni, lakini swali ni je nini kitafanyika baada ya harakati hizi? Hatua itakayofuata ni Rais kuandaa ukabidhi wa miji iliyokombolewa kwa majeshi ya Afrika na kuhakikisha uthabiti wa miji hiyo, kwa maandalizi ya uchaguzi mkuu.

JOHN KERRY ASHIKA NAFASI YA HILLARY CLINTON

Seneta wa zamani nchini Marekani John Kerry ameapishwa kushika nafasi ya Waziri wa Mambo ya Nje wa taifa hilo kubwa duniani. Kerry anachukua nafasi iliyoachwa wazi na waziri aliyemaliza muda wake Hillary Rodham Clinton ambaye aliitumikia wizara hiyo katika utawala wa muhula wa kwanza wa miaka minne wa Rais Barack Obama. Siku ya mwisho ya Clinton katika wadhifa huo ilimalizika kwa mashambulizi dhidi ya ubalozi wa nchi hiyo kwenye mji mkuu wa Uturuki,  Ankara. Mripuaji pamoja na mlinzi wa ubalozi huo raia wa Uturuki wote waliuawa. Taasisi za kidiplomasia za Marekani nchini Uturuki zimekuwa zikilengwa mara kwa mara na makundi ya kigaidi. Mwaka 2008, shambulizi lililofanywa nje ya Ubalozi mdogo wa Marekani mjini Instanbul liliuwa askari polisi watatu pamoja na washambuliaji watatu. Shambulio hilo linaelezwa kufanywa na wanamgambo wenye mafungamano na kundi la al-Qaeda.