Wednesday, December 12, 2012

ABDUL JALIL AWEKEWA KIZUIZI CHA KUTOKA NJE YA NCHI

Waendesha  mashtaka   wa  mahakama  ya  kijeshi  nchini Libya  leo wameweka   marufuku  ya  kusafiri  dhidi  ya Mustafa Abdul Jalil, kiongozi  wa zamani wa Baraza  la Taifa  la  Mpito  ambalo  liliitawala   nchi  hiyo  baada  ya kuondolewa  madarakani  kwa  Muammar Gaddafi. Hatua hiyo  imechukuliwa ukisubiriwa  uchunguzi  kuhusiana  na kifo  cha  kamanda  wa  waasi, Jenerali Abdel Fattah Younes,  ambacho  hakijapatiwa  maelezo. Abdul Jalil aliongoza  baraza  la  taifa  la  mpito  hadi  pale lilipokabidhi  madaraka  kwa  bunge  lililochaguliwa  hapo Agosti mwaka  huu. Anatarajiwa  kufikishwa  mbele  ya mahakama  ya  kijeshi  Februari  20  mwakani  kujibu maswali  yanayohusiana  na  kuuwawa  kwa  Jenerali Younes. Younes, ambaye  alikuwa  waziri  wa  mambo  ya ndani  wa   serikali  ya  Gaddafi , alijitoa  kutoka  serikali hiyo  na  kujiunga  na  vuguvugu  la  mapambano  ya silaha   ambalo  hatimaye  liliuondosha  madarakani utawala  wa  miaka  42  wa  Gaddafi  mwaka  jana. Younes aliuwawa  Julai  2011  katika  mazingira  ambayo  si  ya kawaida  baada  ya  kutakiwa  kuondoka  kutoka  katika mstari  wa  mbele  wa  mapambano   kwa  ajili  ya  kuhojiwa na  maafisa  wa  mapinduzi.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO