Shirika la habari la China limesema kuwa nchi hiyo imeanza ujenzi wa kinu kipya cha kinuklia kwa ajili ya kujipatia nishati, baada ya hatua ya kuzuwia ujenzi kwa muda kufuatia maafa yaliyotokea Fukushima nchini Japan. Shirika la habari la Xinhua limesema kuwa kinu hicho cha nishati kitakachogharimu euro milioni 365 katika mji wa pwani ulioko mashariki mwa nchi hiyo katika jimbo la Shandong, kitakuwa na vifaa vya usalama vya hali ya juu vilivyotengenezwa na watafiti wa China. China ni nchi inayotumia nishati nyingi duniani na nishati ya kinuklia ni muhimu katika juhudi za nchi hiyo kuzuwia mahitaji yanayoongezeka kwa matumizi ya vyanzo vingine kama mafuta. China ilisitisha uidhinishaji wa vinu vipya vya nishati kufuatia tetemeko la ardhi nchini Japan mwaka 2011 na Tsunami iliyoharibu mtambo wa kinuklia wa Fukushima. Hatua hiyo ya usitishaji wa ujenzi iliondolewa mwezi Oktoba.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO