Monday, January 07, 2013

TAMKO LA ASSAD KATIKA MKUTANO WAKE

Rais Bashar al Assad wa Syria amezitaka nchi za eneo na za Magharibi kuacha kuwafadhili kifedha na kisilaha waasi nchini humo ili kutoa mwanya wa kutekelezwa juhudi mpya za kusaka amani nchini humo. Rais wa Syria amezituhumu nchi za Magharibi kwa kufanya njama za kuwapokonya wananchi wa Syria uhuru wao na kuitumbukiza nchi hiyo katika hali ya mchafukoge. Mbali na kuzilaumu nchi za Magharibi kwa kufanya njama za kuwapokonya Wasyria uhuru wao Rais Bashar al Assad amesema kuwa serikali na wananchi wa Syria kamwe hawatatoa mwanya kwa nchi hizo kufanikisha mipango iliyo nje ya uhuru na haki ya kujitawala wananchi hao. Rais Assad ameeleza namna serikali ya Syria inavyokaribisha mpango wowote wa ndani na nje wenye nia njema na taifa hilo utakaosaidia kurejeshwa amani na utulivu huko Syria sambamba na kutatua mgogoro unaoikabili nchi hiyo na kusisitiza kwamba, Syria inaafiki mpango wowote ule ambao utadhamini maslahi ya taifa hilo. Rais Bashar al Assad wa Syria amesema wananchi wa nchi hiyo ambao wana ustaarabu mkongwe ndio pekee wenye haki ya kuchukua maamuzi na ndio wanaopaswa kuainisha mustakbali wa nchi yao kwa kushiriki kwenye masanduku ya kupigia kura.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO