Mazungumzo kati ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na waasi wa M23 yanatarajiwa kuendelea tena leo mjini Kampala, Uganda. Mazungumzo hayo yanaendelea tena ikiwa ni duru nyingine baada ya kusimama kwa muda wa wiki mbili kupisha sherehe za Krismasi na mwaka mpya.
Wawakilishi wa pande mbili ambao tayari wamewasili mjini Kampala, Uganda wamekutana kwa nyakati tofauti na Dakta Crispus Kiyonga Waziri wa Ulinzi wa Uganda ambaye ndiye msimamizi wa mazungumzo hayo. Lengo hasa la mazungumzo hayo ni kutafuta njia za kuhitimisha mgogoro wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambapo kuzorota amani na uthabiti katika maeneo hayo kumesababisha maelfu ya raia kuyakimbia makazi yao. Wakati huo huo, kundi la waasi wa M23 limetahadharisha kuwa, huenda mazungumzo hayo yenye lengo la kusitisha mapigano yakakwama iwapo serikali ya Kinshasa itapinga mapendekezo yaliyotolewa na waasi hao kuhusiana na usitishaji vita.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO