Mapigano makali yaliyotokea katika mji wa Gedo nchini Somalia baina ya wanamgambo wa Al- Shabab na vikosi vya serikali vikisaidiwa na wanajeshi wa Ethiopia yamepelekea kuuawa zaidi ya wapiganaji 14 wa kundi hilo la waasi. Hayo yameelezwa na maafisa wa serikali ya Somalia.
Taarifa zaidi zinasema, mapigano hayo yametokea katika kijiji kimoja kilichoko baina ya miji miwili ya Luuq na Garbaharey iliyoko umbali wa kilomita 100 kutoka mpaka wa Somalia na Kenya na Ethiopia. Afisa mmoja wa serikali ya Somalia ameripotiwa akisema kwamba, kwa sasa vikosi vya serikali viko katika hatua ya mwisho ya kuwafurusha Al-shabab kutoka mjini.
Hata hivyo msemaji wa wanamgambo wa Al Shabab Sheikh Ali Mahmud Rage amesema kuwa, wapiganaji wao wameteketeza magari matatu ya kijeshi na kuua askari kadhaa wa serikali katika mapigano hayo. Ameongeza kuwa, wapiganaji wao wangali wako katika kila kona ya Somalia.

No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO