Tuesday, January 01, 2013

UFARANSA YAANDAA JARIDA LA KUMVUNJIA HESHIMA MTUME (saw)


Jarida la Charlie Hedbo linalochapishwa nchini Ufaransa linakusudia kuchapisha toleo jipya ambalo litakuwa maalumu likiwa na picha zinazomfanyia istihizai na tashtiti Mtume Mtukufu Muhammad SAW.
Taarifa zilizotolewa na jarida hilo zinasema kuwa, toleo hilo maalumu litatoka siku ya Jumatano ijayo likiwa na picha mpya zinazomvunjia heshima Mtume Mtukufu SAW. Jarida hilo liliwahi kuchapisha picha zinazomvunjia heshima Mtume Mtukufu SAW mwezi Septemba mwaka huu na kuibua wimbi la hasira katika nchi za Kiislamu.
Vitendo vya kumvunjia heshima Mtume Mtukufu SAW vimekuwa vikiongezeka kwa kasi katika nchi za Magharibi kwani miezi michache iliyopita ilionyeshwa filamu inayomvunjia heshima Mtume SAW nchini Marekani na kukabiliwa na wimbi la hasira za Waislamu kutoka pembe zote za dunia. Hali kadhalika mwaka 2006 jarida moja la Denmark lilichapisha vikatuni vinavyomvunjia heshima Mtume SAW na kusababisha watu wasiopungua 150 kuuawa katika pembe mbalimbali duniani kwenye maandamano ya kulalamikia uchorwaji wa vikatuni hivyo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO