Saturday, January 05, 2013

MHISPANIA AJIUCHOMA MOTO KWA UGUMU WA MAISHA

Raia mmoja wa Uhispania amechukua uamuzi wa kujiteketeza moto kutokana na kukabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi na kimaisha. Duru za hospitali zimetangaza kuwa, Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 57 aliamua kujiua hapo jana kwa kujichoma moto  katika mji wa Malaga, na kufariki dunia muda mfupi baada ya kufikishwa kwenye hospitali ya Seville. Hali kadhalika ajuza mwengine mwenye umri wa miaka 63 alijiua katika mji wa Malaga siku ya Alhamisi kutokana na kukabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi inayotokana na kutokuwa na kazi. Vitendo vya kujiua kwa raia wa Uhispania vinazidi kuongezeka kutokana na matatizo ya kifedha na ukosefu wa ajira. Wizara ya Kazi na Huduma ya Jamii ya Uhispania hivi karibuni imetangaza kuwa, mwaka 2012 watu wasiopungua 426,364 walipoteza ajira zao nchini humo. Wizara ya Kazi na Huduma ya Jamii  imeeleza kuwa, zaidi ya Wahispania milioni tano na laki nane hawana kazi nchini humo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO