Saturday, January 05, 2013

MATESO BAHRAIN KARIBU KUFIKIA

Mjumbe wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Siasa za Kigeni wa Bunge la Iran amesema kuwa, siasa za ukandamizaji na utesaji zinazofanywa na utawala wa Aal Khalifa nchini Bahrain dhidi ya waandamanaji nchini humo zitafikia ukingoni. Ahmad Bakhshayesh Ardistani ameongeza kuwa, utawala wa Aal Khalifa umefika tamati na wala hauna uwezo wa kujinasua kwenye kinamasi hicho. Ameongez akuwa, utawala wa Aal Khalifa unajinadi kwa kutetea haki za binadamu, huku ukiendeleza wimbi la utesaji dhidi ya wafungwa na  mauaji dhidi ya wananchi wasio na hatia, katika hali ambayo watekelezaji wa jinai hizo hawachukuliwi hatua za kisheria. Akielezea mashirikiano ya pande zote za madola ya Magharibi kwa utawala kandamizi wa Aal Khalifa wa Bahrain, Mjumbe wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Siasa za Kigeni wa Bunge la Iran amebainisha kuwa, baada ya kujitokeza harakati ya kimapinduzi nchini Bahrain, wataalamu kutoka Scotland Yard nchini Uingereza walitumwa nchini Bahrain kwa shabahaa ya kutoa ushauri kwa vikosi vya usalama vya nchi hiyo jinsi ya kukabiliana na maandamano ya wananchi yaliyo dhidi ya utawala wa kifalme nchini humo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO