Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ametaka kutumiwa jina la nchi ya Palestina badala ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina katika balozi zote za Palestina.
Shirika la habari la Palestina WAFA limeripoti kuwa, agizo hilo la Mahmoud Abbas limechukuliwa katika fremu ya mipango yake ya serikali hiyo ya kuiarifisha Palestina kama nchi. Nchi wanachama wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 29 mwezi Novemba mwaka jana ziliafiki kupandishwa hadhi ya Palestina katika Umoja wa Mataifa na kuwa serikali mtazamaji isiyo mwanachama licha ya mashinikizo ya Marekani na utawala wa Kizayuni.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO