Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran leo ameonana na Rais Thomas Yayi Boni wa Benin na kumkabidhi ujumbe wa Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Mwandishi wa Radio Tehran ameripoti habari hiyo kutoka Cotonou, mji mkuu wa Benin na kuongeza kuwa, katika ujumbe wake huo, Rais Ahmadinejad amemwalika Rais wa Benin kutembelea Iran. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran yuko safarini katika nchi kadhaa za Afrika kwa ajili ya kuimarisha uhusiano na nchi hizo.
Hivi sasa Iran ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote NAM. Dk. Ali Akbar Salehi pia amemwambia Rais wa Benin kuwa Iran Ina hamu ya kuona uhusiano wa Tehran na Cotonou unaimarika katika nyanja zote. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anamaliza safari yake leo Jumapili nchini Benin na akitoka nchini humo ataelekea katika nchi nyingine ya magharibi mwa Afrika, yaani Ghana.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO