Saturday, January 05, 2013

WANAJESHI WA NATO WAWASILI UTURUKI

Wanajeshi wa Marekani wanaotarajia kushughulukia mizinga ya makombora ya Patriot iliyopelekwa Uturuki na Jumuiya ya Kujihami ya NATO kuihami nchi hiyo na kusambaa kwa machafuko ya Syria wameshawasili Ankara. Askari hao wametangulia wakati mizinga yenyewe ya Patriot itafuata hapo baadae. Kiasi ya maafisa 400 wa kijeshi wa Marekani watawasili siku chache zijazo na mizinga hiyo ya makombora ya Patriot kwa ndege za kijeshi za nchi hiyo. Kwa mujibu wa taarifa kutoka mtandao wa jeshi la Marekani makao makuu ya kijeshi ya Ulaya, maafisa hao ni wa kikosi cha pili cha masuala ya anga pamoja na cha tatu cha mizinga ya makombora ya Patriot vinavyotoka kwenye kambi ya jeshi ya Oklahoma. Makombora  mingine ya Patriot kutoka Ujerumani na Uholanzi yatafika Uturuki katika kipindi cha wiki kadhaa zijazo. Vikosi vya Marekani vilivyowasili Uturuki katika kambi ya jeshi ya la anga ya Incirlik watasimamia mizinga miwili kati ya sita ambayo imeahidiwa na jumuiya ya NATO. Uturuki iliomba rasmi msaada wa kijeshi kutoka jumuiya ya NATO ambayo yenyewe ni mwanachama mwezi Novemba mwaka jana ili kuimarisha ulinzi katika eneo la mpaka baina yake na Syria ambalo limeathiriwa na vita vinavyoendelea kati ya serikali na waasi.  

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO