Sunday, February 17, 2013

IRAN YAKOSOA VIKALI MATAMSHI YA BAN KI MOON


Mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwenye Umoja wa Mataifa amekosoa vikali matamshi ya Ban Ki moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusiana na mpango wa nyuklia wa Iran wenye malengo ya amani na kusisitiza kuwa, misimamo ya upendeleo ya Ban Ki moon inakinzana na uwajibikaji wa katibu mkuu huyo. Toleo la jana la gazeti la Washington Post linalochapishwa nchini Marekani  limemnukuu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akidai  kuwa, Iran inaweza kustafidi na mazungumzo ya nyuklia chini ya kalibu ya Umoja wa Mataifa iwapo itafumbia macho mpango wake wa kutengeneza bomu la atomiki. Muhammad Khazaei amelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutoa jibu la haraka kuhusiana na matamshi hayo yasiyokuwa ya uwajibikaji ya Ban Ki moon na kusisitiza kuwa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anapaswa kutumia njia za kidiplomasia na za mazungumzo kwa lengo la kutatua migogoro na siyo kuupotosha ulimwengu. Mara kadhaa viongozi wa Iran wamesisitiza kuwa, miradi ya nyuklia hapa nchini inafanyika kwa malengo ya amani na chini ya usimamizi wa wa wakala wa IAEA.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO