Sunday, February 17, 2013

WANASIASA PAKISTAN WATAKA MAZUNGUMZO NA TALIBAN


Viongozi wa kisiasa wa Pakistan wametoa wito wa kufanywa haraka mazungumzo ya amani na kundi la Taliban. Wito huo umetolewa katika Kongamano la Makundi Yote (APC) lililofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo Islamabad. Taarifa zinasema kuwa vyama 27 vya kisiasa vilishiriki kwenye kongamano hilo la siku moja lililoitishwa ili kujadili uwezekano wa kufanya mazungumzo na kundi la Taliban. Viongozi hao wamesisitiza kuwa kipaumbele cha kwanza ni kufanya mazungumzo na wanamgambo ili kurejesha amani nchini Pakistan. 
Katika wiki za hivi karibuni kumekuwa kukitolewa kwa wingi wito wa kufanywa mazungumzo ya amani, huku pande za serikali na wanamgambo pia zikionyesha hamu ya kufanya mazungumzo hayo. Tarehe 5 Februari Waziri wa Mambo ya Ndani wa Pakistan Rehman Malik alisema kwamba, nchi yake iko tayari kufanya mazungumzo ya kusaka amani na wanamgambo wa Taliban.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO