Thursday, February 14, 2013

MAZISHI YA SHEIKH NASSOR BACHU

Mwili wa Sheikh na ulamaa wa tanzania Sheikh Nassor Bachu wastiriwa leo katika makaburi Donge huko Zanzibar. Swala ya mauti ilishindikana kufanyika katika msikiti uliopangwa mwanzo kutokana na umati wa waumini waliofurika kumsitiri Sheikh huyo na hivyo kufanyika katika viwanja vya Maisara. Wengi wa masheikh mbalimbali wa Afrika Mashariki walishirikiana na waumini mbalimbali katika ibada hiyo na hatimaye kuikamilisha safari yake ya kwanza ya kuelekea Akhera.
Kwa mujibu wa duru mbalimbali za habari miongoni mwa viongozi wa juu wa serikali walioshirki ni Makamu wa rais Maalim Seif Sharif huku viongozi wengine wakiwa katika shughuli mbalimbali za kidunia na hatimaye hadi kushindwa kumzika gogo hilo la Ilmu ya dini ya kiislam kwa kufuata Sunna Sahih ya Mtume Muhammad Swallal lahu alayhi wasallam.
Pia duru nyinginer za habari zikionyesha kuwa Rais Kikwete yuko Moshi katika maziko ya askofu ASKOFU ALMEDEUS PETER MSARIKIE.
 
Picha za matukio mbalimbali ya maziko ya sheikh Nassor






 

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO