Thursday, March 07, 2013

UN YALAANI KUTEKWA NYARA ASKARI WAKE

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali kitendo cha waasi wa Syria wanaoungwa mkono na nchi za Magharibi cha kuwateka nyara askari wa kulinda amani wa umoja huo katika milima ya Golan inayokaliwa kwa mabavu na Israel. Taarifa ya wanachama 15 wa baraza hilo imesema, nchi wanachama zinalaani kutekwa nyara kundi la zaidi ya askari 20 wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa (UNDOF) huko Golan na imetaka waachiliwe huru haraka.
Naibu msemaji wa Umoja wa Mataifa Eduardo del Buey amethibitisha kuwa askari hao wameshikwa na kusema kuwa walikuwa katika shughuli zao za kawaida ambapo walisimamishwa na kundi la watu wenye silaha na kukamatwa. Katika video iliyorushwa kwenye internet waasi hao wamesikika wakisema kwamba, hawatawaachilia huru askari hao wa Umoja wa Mataifa hadi pale vikosi vya serikali ya Syria vitakapoondoka katika kijiji cha Jamla karibu na eneo hilo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO