Friday, March 08, 2013

BINGWA WA MBIO ZA MARATHON ASHINDA UBUNGE KENYA

Mkimbiaji Wesley Kipchumba Korir wa Kenya bingwa wa mbio za Boston Marathon za  mwaka 2012 wiki hii andika historia mpya katika  uwanja wa siasa baada ya kunyakua ushindi wa kiti cha ubunge wa Cherengany katika uchaguzi mkuu nchini Kenya uliofanyika siku ya Jumatatu iliyopita. Korir 28 ambaye alitumbukia kwenye kinyang'anyiro hicho akiwa mgombea binafsi alisema kuwa, alikuwa anapenda sana kuwa mwanasiasa tokea akiwa mdogo, lakini alikuwa akisubiri fursa ili aweze kujitumbukiza rasmi kwenye ulingo huo. Wesley Korir ambaye aliishi Marekani  kwa ajili ya  masomo  ya elimu ya juu, mwaka jana aliibuka mshindi wa medali ya dhahabu katika mashindano ya mbio za Boston Marathon  baada ya kutumia muda wa masaa 2: dk 12 sekunde 40. Mkimbiaji huyo amesema kuwa, licha ya kuwahudumia wananchi wa eneo lake bungeni, ataendelea pia kushiriki kwenye michuano mbalimbali ya mbio za Marathon. Wesley Korir amethibitisha kwamba atashiriki kwenye michuno ya mbio za Boston Marathon zitakazofanyika mwezi Aprili mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO