Mwandishi mashuhuri wa fasihi barani Afrika, Profesa Chinua Achebe amefariki dunia. Habari za kifo chake zimetolewa na duru mbalimbali ikiwemo matibaa inayochapisha vitabu vyake ya Penguin yenye makao yake mjini London, Uingereza.
Duru za karibu na familia ya msomi huyo raia wa Nigeria zimesema Achebe amefariki dunia katika hospitali moja mjini Boston katika jimbo la Massachusetts nchini Marekani akiwa na umri wa miaka 82. Profesa Chinua Achebe alianza kupata umashuhuri zaidi ya miaka 50 iliyopita alipoandika kitabu chake cha kwanza kiitwacho 'Things Fall Apart' ambacho kinazungumzia ukoloni kwa mtazamo wa Waafrika.
Serikali nyingi za kiimla barani Afrika ziliwahi kupiga marufuku vitabu vya msomi huyo kutokana na mbinu ya uandishi inayoanika wazi uozo ndani ya makasri ya viongozi na jinsi madaraka yanavyomfanya mtu kuwa gwiji wa maasi yote duniani.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO