Rais wa Palestina Mahmoud Abbas amemtaka Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu awasilishe mpango juu ya taifa la siku zijazo la Wapalestina, kabla ya kuanza tena kwa mazungumzo yoyote ya amani. Msaidizi wa kiongozi huyo wa Palestina, Nimr Hammad, aliliambia shirika la habari AFP kwamba Abbas anataka kujua kutokana na ramani ambayo Netanyahu atamkabidhi Waziri wa Nje wa Marekani John Kerry, nini maoni ya waziri mkuu huyo kuhusu suluhisho la kuwa na dola mbili na hasa suala la mipaka. Matamshi ya Rais huyo wa Palestiana yamekuja siku kadhaa kabla ya ziara ya Waziri Kerry ambaye atakua na mazungumzo ya wiki mbili na viongozi wa Israel na Palestina, akijaribu kuyafufua mazungumzo ya amani yaliyokwama.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO