Kiasi ya wakimbizi 35,000 wa Syria wamerejea nyumbani kutoka Jordan, tangu kuzuka mgogoro nchini mwao mwezi Machi 2011, lakini idadi kubwa imejiunga na wimbi hilo la wakimbizi mwezi uliopita pekee. Msemaji wa serikali ya Jordan anayehusika na wakimbizi, Anmar al-Hammud, amesema wakimbizi wa Syria 34,824 wamerejea nyumbani na kwamba miongoni mwao 2,500 wamerudi kwa hiyari Alhamisi, kutoka kambi ya wakimbizi ya Zaatari, kaskazini mwa Jordan, kwa msaada wa idara za usalama za Falme hiyo. Jordan inasema imewapokea zaidi ya wakimbizi 475,000 kutoka Syria.
Zaidi ya wakimbizi 41,000 waliingia Jordan mwezi Machi pekee na nchi hiyo inahofia huenda idadi ikaongezeka hadi 700,000 ifikapo mwisho wa mwaka huu. Kwa mujibu wa Kamishna wa Umoja wa Mataifa anayehusika na wakimbizi, Wasyria milioni 1.2 wamekimbilia nchi za jirani katika kipindi cha miaka miwili iliopita.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO