Wizara ya Ulinzi ya Marekani 'Pentagon' imemfuta kazi Meja Jenerali Ralph Baker Kamanda wa Majeshi ya Marekani katika eneo la Mashariki na Pembe ya Afrika baada ya kukumbwa na kashfa ya ubakaji na udhalilishaji wa kijinsia barani humo. Meja Robert Freeman Msemaji wa Pentagon amesema kuwa, Meja Jenerali Baker ambaye alikuwa akiviongoza vikosi vya Marekani katika eneo hilo lenye makao yake nchini Djibouti, ametimuliwa baada ya Jenerali Carter Ham Kamanda wa Vikosi vya Marekani barani Afrika AFRICOM kutoa amri hiyo. Jenerali Carter Ham alitoa amri hiyo wakati ulipokuwa umesalia muda mchache kabla ya kumkabidhi hapo jana Jenerali David Rodriguez ukamanda wa vikosi vya Marekani barani Afrika.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO