Saturday, April 06, 2013

WAISLAM WAZIDI KUPATA MATESO UFARANSA

Polisi katika mji wa Voiron ulioko kusini mashariki mwa Ufaransa jana ilielezea kufutwa picha za misalaba minne iliyochorwa kwenye kuta za Msikiti mmoja ulioko mjini humo. Polisi ya mji huo imeeleza kuwa, uchunguzi umeanza wa kubaini wahusika wa tukio hilo la kuchora misalaba kwenye kuta za Msikiti. Mkuu wa Taasisi za Misikiti nchini Ufaransa amekosoa vikali vitendo hivyo na kusisitiza kwamba vitendo vya kuvunjia heshima matukufu ya dini nyinginezo havikubaliki. Kabla ya hapo, Kitengo cha Usimamizi  cha Baraza la Utamaduni la Waislamu la Ufaransa CFCM kimeeleza kuwa, takwimu zinaonyesha kuongezeka vitendo vya  chuki na uadui dhidi ya Uislamu mwaka 2012 nchini humo, licha ya  viongozi  wa baraza hilo kuitaka serikali ya Kisoshalisti ya Ufaransa kukabiliana na vitendo hivyo vya kibaguzi.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO