Mamlaka ya
mawasiliano ya Saudi Arabia imetishia kufunga matumizi ya “Whatsapp, Skype na
Viber”. Mamlaka hiyo inataka “applications”
hizo zifuate kanuni na sheria sahihi za nchi hiyo japokuwa mamlaka hiyo
haijasema ni sheria gani za kufuatwa na wala haijafafanua ni sheria zipi
zilizovunjwa na matumizi ya “application” hizo. Wiki iliyopita mitandao yote
inayoendesha mawasiliano ya simu iliombwa na serikali ya Saudi Arabia kuachia mitandao
yote ya mawasiliano iendeshwe na mamlaka ya mawasiliano. Kutokana na mmiliki wa
blog nchini Saudi Arabia anadhani kuwa uamuzi huo huenda unatokana na
maandamano yaliotokea hivi karibuni nchini humo na inawezekana waandamanaji wanatumia
“application” hizo kufanikisha maandamano hayo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO