Serikali ya Zimbabwe imetangaza kuwa, inapinga mpango wa kutumwa wasimamizi wa kimataifa wa uchaguzi ujao wa rais katika nchi hiyo. Taarifa ya serikali ya Zimbabwe imebainisha kwamba, haikubaliani na pendekezo la Marekani la kutumwa waangalizi wa kimataifa katika uchaguzi ujao wa rais nchini humo na mkabala wake ifutiwe vikwazo. Awali Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayesimamia masuala ya Afrika Johnnie Carson aliwaandikia barua Makamu wa Rais na Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Zimbabwe akiitaka Harare ikubali kutumwa waangalizi wengi wa ndani na wa kimataifa kwa ajili ya kusimamia uchaguzi mkuu ujao. Johnnie Carson alisisitiza katika barua yake hiyo kwamba, kama Zimbabwe itaafiki suala hilo, basi serikali ya Washington iko tayari kutazama upya vikwazo vyake dhidi ya nchi hiyo ya Kiafrika na kuchukua hatua za kupunguza makali yake. George Charamba, Msemaji wa Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amesisitiza kwamba, Harare haikubaliani na pendekezo hilo la Marekani.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO