Tuesday, April 09, 2013

ZAIDI YA WANAHARAKATI 50 WAWASILI GHAZA


Wanaharakati wa kimataifa zaidi ya 50 wanatarajiwa kuwasili katika Ukanda wa Ghaza huko Palestina leo lengo likiwa ni kuonyesha mshikamano na wakazi wa ukanda huo unazongirwa kiuchumi. Wakiwa huko Ghaza wanaharakati hao wa kimataifa watazitembelea pia taasisi za Unrwa (shirika la misaada ya wakimbizi wa Kipalestina).
Wakati huo huo wavuvi wa Kipalestina wamegoma wakilalamikia hatua ya utawala haramu wa Kizayuni ya kuwapunguzia eneo lao la uvuvi katika pwani ya Ukanda wa Ghaza. Mamia ya wavuvi wa Kipalestina leo wamegoma kupanda boti zao za uvuvi katika maji ya pwani ya Palestina katika bandari ya Ghaza wakilalamikia uamuzi wa Israel wa kuwapunguzia eneo la kuvulia samaki kutoka maili sita hadi tatu.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO