Ethiopia imepuuzia matamshi ya kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya bwawa kubwa linalojengwa katika mto Nile kuwa ni vita vya kisaokolojia na kusema kuwa nchi hiyo itajilinda na kuendelea na mradi huo bila kujali lolote.
Vita vya maneno kati ya nchi hizo mbili ambazo zinauchumi unaokuwa kwa haraka zaidi vimezusha hofu ya kuingia katika mzozo wa maji, licha ya kuwa pande zote mbili pia zinatafuta muafaka wa kidiplomasia kuhusiana na mradi huo mkubwa kabisa wa uzalishaji wa umeme unaotumia maji ya mto Nile katika bara hilo.
Akijibu hotuba iliyotolewa Jumatatu na rais Mohammed Mursi , ambapo alisema Misri haitaki vita , lakini itaweza fursa zote wazi kuzuwia kupoteza kiasi chochote cha maji, msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya Ethiopia amesema majivuno ya aina hiyo hayataweza kubadilisha msimamo wa nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO