Wednesday, June 12, 2013

UMOJA WA MATAIFA WASEMA M23 INASAJILI WATOTO

Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inalituhumu kundi la waasi la M 23 kuwasajili watoto 53 katika jeshi lake tuhma ambalo kundi hilo la waasi wanasema ni propaganda. Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ban Ki Moon nchini humo anayemaliza muda wake Roger Meece amethibitisha kuwepo kwa watoto hao katika kundi hilo na kuongeza kuwa wana ushahidi wa kuthibitisha hilo. Hata hivyo, uongozi wa kundi la M 23 Bertrand Bisimwa unakanusha madai hayo ya Umoja wa Mataifa na kusema kuwa sheria za kundi hilo haliwaruhusu watoto kujiunga katika kundi lao.
Bisimwa ameongeza kuwa lengo la Ofisi ya Umoja wa Mataifa ni kuwapaka tope na ni propaganda dhidi yao. Katika hatua nyingine, shirika la Umoja wa mataifa linaloshughulikia watoto duniani UNICEF linataka waasi hao kuacha kuwasajili watoto katika kundi hilo. Dan Rolon kiongozi wa kitengo cha habari katia shirika hilo ameimabia RFI Kiswahili kuwa watoto wamekuwa wakiwekwa katika mstari wa mbele wakati wa mapambano dhidi ya wanajeshi wa serikali. Siku ya Jumatatu Ban Ki Moon alimteaua Martin Kobler Balozi kutoka kutoka Ujerumani kuwa mwakilishi wake mpya nchini humo na kuongoza majeshi ya kulinda amani ya MONUSCO.
MONUSCO ambayo ina wanajeshi zaidi ya 17,000 pamoja na wale wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, Malawi na Afrika Kusini wameanza harakati za kupiga doria katika ngome za waasi wa M 23. Kundi la M 23 kwa uapnde wao walitangaza juma lililopita kuwa wametuma ujumbe wake jijini Kampala Uganda kuendelea na mazungumzo ya amani na serikali ya Kinsasha na kupata suluhu la kisiasa kuhusu mgogoro wa nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO