Wizara ya Mafuta ya Sudan imeiandikia rasmi serikali ya Sudan Kusini kuitaarifu kwamba imenza kufunga mabomba ya mafuta ili kuzuia usafirishaji wa mafuta ghafi kutoka Kusini kwenda mjini Khartoum. Kwenye barua hiyo, Serikali ya Sudan imesema hatua hiyo imechukuliwa ili kuilazimisha Sudan Kusini kusitisha uungaji mkono wake kwa makundi ya waasi wanaolenga kumpindua rais Omar Hassan al-Bashir. Khartoum imesema ufungaji wa mabomba hayo utafanywa hatua kwa hatua katika kipindi cha siki 60 ili kuepusha uharibifu wa mazingira. Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan imesema iwapo serikali ya Juba itaonyesha nia njema na kusimamisha misaada yake kwa waasi, basi Khartoum italifikiria upya suala hilo na pengine kuamua kuruhusu tena mafuta kusafirishwa kupitia mabomba yake. Kwa sasa Sudan Kusini ndiyo inayozalisha mafuta mengi ya petroli lakini viwanda vya kusafisha mafuta hayo viko Sudan na hata mabomba ya kusafirishia mafuta hayo kutoka Kusini kwenda Kaskazini yanamilikiwa na Khartoum.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO