Sunday, July 07, 2013

ARAB LEAGUE YAKOSOLEWA JUU YA MISIMAMO YAKE

Waziri wa Mambo ya Nje wa Lebanon, Adnan Mansour amekosoa misimamo ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kuhusu kadhia ya Syria na kusema kosa la kwanza la jumuiya hiyo ni kuegemea upande mmoja kwenye mgogoro huo. Mansour amekumbusha kuwa, ni vigumu kwa mtu anayeegemea upande mmoja wa mgogoro kutoa jibu muafaka la kutatua mgogoro huo. Waziri wa Mambo ya Nje wa Lebanon amesema Syria ni nchi huru na kwamba uingiliaji wa mambo yake ya ndani ni ukiukaji wa sheria za kimataifa. Adnan Mansour ameongeza kuwa, Mgogoro wa Syria unaweza kutatuliwa na Wasyria wenyewe pasina mashinikizo kutoka nje. Hata hivyo ametahadharisha kwamba misimamo ya baadhi ya nchi za Kiarabu huenda ikazidi kuitumbukiza Syria katika machafuko na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Akitoa mfano wa jinsi vita hivyo vinavyoendelea kusambaa hadi Lebanon, Mansour amesema mgogoro huo usipotatuliwa kwa njia za amani, utakuwa na athari mbaya katika eneo zima la Mashariki ya Kati.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO