Watu kadha wamejeruhiwa wakati bomu lililotegwa katika gari liliporipuka katika kitongoji cha kusini mwa mji wa Beirut leo, sehemu ambayo ni ngome kuu ya kundi la wanamgambo wa Kishia la Hezboullah ambalo limeingilia kati mapigano katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria.
Wasi wasi umetanda nchini Lebanon kufuatia kundi hilo la wanamgambo kuingilia kati mapigano nchini Syria wakisaidia upande wa rais wa nchi hiyo Bashar al-Assad, ambaye majeshi yake yanapambana na uasi uliodumu miaka miwili sasa ukiongozwa na Waislamu wa madhehebu ya Sunni ambao ndio wengi nchini humo.
Wingu la moshi mweusi lilikuwa linatoka katika jengo linaloishi watu wengi katika kitongoji hicho cha kusini mwa mji mkuu Beirut. Eneo hilo lenye maduka mengi huenda lilikuwa limejaa watu leo, siku ya mwanzo ya mfungo wa Ramadhan.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO