Friday, May 31, 2013

BREAKING NEWS: MATOKEO KIDATO CHA SITA 2013



MAREKANI: IRAN YAONGEZA MISAADA YA KIGAIDI

Iran imeongeza msaada wake kwa makundi ya kigaidi, na nguvu za mtandao wa kigaidi wa Al-Qaida zimepungua- haya yametajwa katika ripoti ya mwaka ya Marekani, juu ya hali ya ugaidi duniani. Wizara ya mambo ya nchi za nje ya nchi hiyo imekitaja kikosi cha walinzi wa mapanduzi cha Irani, wizara ya ujasusi ya nchi hiyo na msada inaoutoa kwa kundi la wanamgambo wa kishia nchini Lebanon, Hizbollah.
Ripoti ya Marekani imesema kuwa msaada wa Iran kwa ugaidi umefika kwenye kiwango ambacho hakijaonekana tangu miaka ya 1990, ikifadhili mashambulizi katika maeneo ya kusini mashariki mwa Asia, Ulaya na Afrika.
 Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mtandao wa al-Qaida ambao kwa muda mrefu ndio ulikuwa shabaha kubwa ya vita dhidi ya ugaidi umeendelea kudhoofika baada ya kuuawa kwa viongozi wake kama Abu Yahya al-Libi na Abu Zaid al-Kuwaiti.

OBAMA ATUMIWA BARUA NYINGINE YENYE SUMU

Shirika la upelelezi la Marekani FBI limesema kuwa barua yenye sumu hatari aina ya ricin ilitumwa kwa rais Barack Obama kutoka Spokane katika jimbo la Washington, siku ile ile barua sumu kama hiyo ilipotumwa kwa Jaji wa mahakama kuu na kwa posta.
Mtu mmoja alikamatwa wiki iliyopita huko Spokane kuhusiana na barua hiyo iliyotumwa kwa jaji, na ambayo ilizuiliwa tarehe 14 mwezi huu wa Mei. FBI imesema barua iliyokuwa imetumwa kwa rais Obama iligunduliwa tarehe 22, na kuongeza kuwa barua nyingine kama hiyo ilikuwa imetumwa kwenye kituo cha ndege za kijeshi kilicho karibu.
Taarifa ya FBI na ya huduma za posta imesema kuwa barua zote 4 ziliwekewa stampu tarehe 13 Mei huko Spokane. Tatu kati ya barua hizo zimethibitishwa kuwa na sumu ya ricin, na nyingine moja bado inachunguzwa.

MASHAMBULIZI YA DRONE ZA MAREKANI HUPANGWA UJERUMANI

Vyombo vya habari vya Ujerumani vimeripoti kuwa mashambulizi ya ndege za Marekani zisizokuwa na rubani barani kiafrika  yamekuwa yakiendeshwa kutoka kituo cha anga cha Ramstein kilichoko katika jimbo la Rheinland Platinate hapa Ujerumani.
Kipindi cha Panorama cha kituo cha Televisheni cha ARD, pamoja na gazeti la Süddeutsche Zeitung vimesema kuwa kituo hicho cha Ramstein ni muhimu katika kuweka mawasiliano kati ya  Marekani na ndege zake hizo wakati zikiwa kwenye mashambulizi barani Afrika.
Kwa mujibu wa gazeti la jeshi la Marekani, operesheni za ndege hizo katika nchi kama Somalia na Yemen haziwezi kufanikiwa bila kituo cha Ramstein. Serikali ya Ujerumani imesema haina habari juu ya hayo yaliyotangazwa na vyombo hivyo vya habari, kwamba mashambulizi hayo yanapangwa na kutekelezwa nchini Ujerumani.

ASSAD YAITISHJIA ISRAEL KWA VITA MPYA

Rais wa Syria Bashar al-Assad ametishia kuanzisha upya mapambano dhidi ya Israel katika milima ya Golan, na kuongeza kuwa Urusi iko tayari kuipa nchi yake mfumo wa kisasa wa kujilinda dhidi ya mashambulizi ya anga. Akizungumza katika mahojiano na kituo cha televisheni cha cha al-Manar kinachomilikiwa na kundi la Hizbollah, Assad amesema kuna miito inayozidi kuongezeka  miongoni mwa wananchi, kutaka Syria iweke harakati mpya za kujilinda katika milima ya Golan.
Hadi sasa, Israel ambayo iliiteka milima hiyo mwaka 1981, haijatoa tamko lolote kuhusu kitisho hicho cha rais Assad. Magazeti ya Vedomosti na Kommersant  ya Urusi yamekanusha uvumi kuwa tayari Urusi imekwishaipa Syria makombora aina ya S-300, na kuongeza kuwa  huenda makombora hayo yasipelekwe Syria mwaka huu. Marekani imeonya kuwa ikiwa Urusi itaipa Syria makombora hayo, hatua hiyo itaufanya  mgogoro wa Syria kuzidi kuwa mbaya.
        

WANACHAMA WA HAMAS NA FATAH WAKUTANA MISRI

Wawakilishi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS na wenzao wa Fat'h wamekutana katika mji mkuu wa Misri, Cairo kwa ajili ya duru nyengine ya mazungumzo, lengo likiwa ni kumaliza hitilafu zilizopo na kuleta umoja baina yao. Kwa mujibu wa Yahya Rabbah, afisa mwandamizi wa harakati ya Fat'h wajumbe wa harakati hiyo na wale wa Hamas walikutana hapo jana huko Cairo ili kufuatilia utekelezaji wa makubaliano ya kuleta maridhiano ya kitaifa kati ya Wapalestina. Rabbah amesisitiza juu ya kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa na kuainishwa tarehe ya kufanyika uchaguzi bila ya masharti yoyote. Vikao vya viongozi wa Fat'h na Hamas vimekuwa vikifanyika katika kalibu ya kuendeleza mashauriano baina ya pande mbili kwa ajili ya kutekeleza makubaliano yaliyosainiwa huko nyuma hususan yale yanayohusiana na uundaji wa serikali ya umoja wa kitaifa na kuainishwa tarehe ya kufanyika uchaguzi huko Palestina. Mnamo mwezi Mei mwaka 2011 huko Cairo, Misri na Februari mwaka uliopita wa 2012 mjini Doha , Qatar, makundi ya Kipalestina yalitia saini hati za mwafaka wa kumaliza hitilafu na kuunda serikali ya umoja wa kitaifa. Hata hivyo hadi sasa mwafaka huo bado haujatekelezwa. Hamas ilishatangaza hapo kabla kuwa imelikubali wazo la kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa ya Palestina itakayoongozwa na Rais wa Mamlaka ya Ndani Mahmoud Abbas na kwamba hivi sasa inasubiri jibu la harakati ya Fat'h. Safari ya hivi karibuni ya Mahmoud Abbas katika Ukanda wa Gaza iliyofanywa kwa lengo la kuleta umoja kati ya eneo hilo na lile la Ufukwe wa Magharibi ilipokewa kwa mikono miwili na viongozi wa Hamas; na hivi sasa Gaza inasubiri kwa hamu hatua muhimu inayopaswa kuchukuliwa na Rais wa Mamlaka ya Ndani ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ili kufungua njia ya kufanyika chaguzi mbili muhimu za bunge la Palestina na Rais wa Mamlaka ya Ndani. Kwa mara ya mwisho uchaguzi wa Rais wa Mamlaka ya Ndani ulifanyika mwaka 2005 na ule wa bunge la Palestina ulifanyika mwaka 2006, na hivi sasa baada ya kupita miaka miwili tangu ulipomalizika muda ulioainishwa kisheria Wapalestina wanasubiri kufanyika uchaguzi mpya katika ardhi zao zinazokaliwa kwa mabavu. Kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa sio tu kutaunganisha safu za Wapalestina bali kutawafungulia njia pia ya kuamua juu ya mustakabali wao wa kisiasa.
Ni wazi kwamba siasa za Marekani za kuchochea mifarakano ndizo zilizokwamisha juhudi za kuleta umoja baina ya Ukanda wa Gaza na Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan. Kutenganishwa Gaza na Ufukwe wa Magharibi kulikofanikishwa kwa njama ya Marekani mnamo mwaka 2007 ndiko kulikozichonganisha harakati za Fat'h na Hamas na kuwadhoofisha Wapalestina katika kukabiliana na njama za utawala wa Kizayuni wa Israel. Utengano huo ndio uliorahisisha pia uendelezaji wa njama ya ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Wapalestina. Katika mazingira kama hayo ambapo Marekani inafanya juu chini kuyafufua tena mazungumzo ya mapatano kati ya Wapalestina na utawala haramu wa Israel kwa gharama yoyote ile huku kukiwepo pia njama hatari za kuundwa eti nchi ya Palestina sambamba na dola la Kiyahudi lisilojumuisha Wapalestina ambao ni wakaazi wa ardhi za Palestina zilizoanza kukaliwa kwa mabavu mwaka 1948, ndipo viongozi wa Hamas wakasisitiza juu ya udharura wa Wapalestina kujihadhari na njama hizo na kuzidisha kasi ya harakati za kufanikisha mpango wa uundaji wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Palestina

ZANA ZA KIVITA ZA HIZBUL LAH ZAPATIKANA NIGERIA

Karakana ya silaha inayoaminika kumilikiwa na kundi la Hezbollah, nchini Lebanon imapatikana Kaskazini mwa Nigeria. Kwa mujibu wa taarifa za jeshi na shirika la ujasusi la Nigeria raia watatu wa Lebanon wamekamatwa. Msemaji wa jeshi, Brigedia Gen Ilyasu Isa Abba, pia amethibitisha hilo.Silaha hizo ikiwemo, risasi, zana za kukinga magari ya kivita dhidi ya mashambulizi na RPG, zilipatikana ktika karakana mjini Kano.
Maafisa wa usalama walisema kuwa silaha hizo zilinuiwa kutumiwa dhidi ya maslahi ya Israel na nchi za Magharibi. Hii ni kazi ya Hezbollah," katibu mkuu wa usalama mjini Kano Bassey Ettang alisema.Na unaweza hata kuwa na uhakika kuwa ikiwa hili linafanyika, inawezekana wanasaidia makundi ya kigaidi wanaoendesha harakati zao nchini humu,'' alidokeza bwana Bassey. Brig Gen Ilyasu Isa Abba alisema kuwa zana 11 za magari ya kivita, guruneti na makombora 21 bunduki 17 aina ya Ak-47 na maguruneti 76 ni baadhi ya silaha zilizopatikana. Mmiliki wa karakana hiyo, ambako silaha zilipatikana, zikiwa zimefichwa chini ya vumbi la mbao, hakuwa nchini humo.
Kuna jamii kubwa ya walebanese wanaofanya kazi mjini Kano, mji wa kibiashara wa Nigeria Kaskazini.
Mji wa Kano eneo la Kaskazini Mashariki mwa Nigeria zimekubwa na mashambulizi ya mara kwa mara katika miaka mitatu iliyopita, tangu wapiganaji wa kiisilamu Boko Haram walipoanzisha harakati zao. Bwana Ettang aliongeza kuwa "unaweza pia kuwa na uhakika kundi kama hili likiwa lipo, inaweza hata kuwasaidia wapiganaji wengine walioko nchini humo.'' Hezbollah ni kundi la Kishia pamoja na kuwa vuguvugu la kisiasa lenye makao yake nchini Lebanon. Linatambulika na Marekani kama kundi la kigaidi. Boko Haram, ambalo jina lake lina maanisha tamaduni za kimagharibi zinapingwa, linasema, nia yake ni kuipindua serikali sasa na kubuni serikali ya kiisilamu. Kuna wasiwasi mkubwa kuwa kundi la Boko Haram huenda linasaidiwa na mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda katika nchi zengine

Thursday, May 30, 2013

ISRAEL YAITISHA RUSSIA KUHUSU MAKOMBORA

Baada ya Russia kuamua kuiuzia Syria mitambo ya kisasa ya kuzuia makombora, Israel imeingiwa na kiwewe na kutoa vitisho dhidi ya Moscow kuhusiana na mpango wake huo ikisema kwamba, iko tayari kutumia mabavu kuzuia Syria kupelekewa makombora hayo. Jana Jumanne Russia ilitangaza kwamba itaendelea na mpango wake waliokubaliana na serikali ya Damascus wa kuipatia Syria mmitambo ya kuzuia makombora aina ya S-300, na kwamba suala hilo litazuia uingiliaji wa wageni katika masuala ya ndani ya Syria. Moshe Ya'alon Waziri wa utawala wa kizayuni wa Israel anayeshughulikia masuala ya kijeshi amedai kuwa, ni wazi suala hilo ni tishio kwao na kutishia kwamba iwapo silaha hizo zitaifikia Syria basi Israel itajua la kufanya

MADAGASCAR YAAKHIRISHA TAREHE YA UCHAGUZI

Serikali ya Madagascar imetoa amri ya kuakhirishwa tarehe ya kufanyika uchaguzi wa Rais na Bunge nchini humo. Serikali ya mpito ya Madagascar jana ilitangaza kuwa, Baraza la Mawaziri limeafiki kuakhirisha tarehe ya uchaguzi wa Rais na Bunge baada ya kufanya vikao kadhaa vya kutafuta njia za kumaliza mgogoro wa kisiasa wa nchi hiyo.
Serikali ya Antananarivo aidha imesisitiza kuwa, tume ya uchaguzi ya Madagascar inawajibika kutayarisha jendwali la kuitisha uchaguzi huo kwa mujibu wa tarehe zitakazotangazwa tena.
Duru ya kwanza ya Uchaguzi wa Rais wa Madagascar ilikuwa imepangwa kufanyika Juni 24 na duru ya pili Septemba 25 mwaka huu pamoja na uchaguzi wa Bunge.

NAFASI MPYA ZA KAZI HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

Hospitali ya taifa Muhimbili (MNH) imetangaza nafasi za kazi kwa wauguzi mbalimbali hapa nchini. Taarifa ya kazi hizo ilitangazwa juzi tarehe 27 JUNE 2013 na mkurugenzi mtendaji wa Hospitali hiyo Dr. Marina Njelekela. Zaidi ya nafasi 450 zimetangazwa. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 21 JUNE 2013, hivyo yawapasa kuchangamkia nafasi hizo. Kwa maelezo zaidi ya kila kitengo na idadi ya wanaohitajika katika vitengo mbalimbali tafadhali  Bofya hapa.........

BREAKING NEWS: MATOKEO MAPYA KIDATO CHA NNE 2012 YATANGAZWA.

Baraza la mitihani nchini Tanzania NECTA baada ya kurudia tena kusahihisha mitihani ya watahiniwa waliohitimu mwaka 2012 sasa yatangaza rasmi matokeo hayo. Baada ya wanafunzi wengi kufeli kwa alama mbaya walizozipata katika mitihani hiyo baraza liliamua kurudia kusahihisha kwani vigezo walivyotumia mwanzo vilikuwa ni vipya ambavyo havikuwa vikitumika huko mwanzo hivyo kufanya wanafunzi wengi kufeli. KW Kwa kuweza kutazama matokeo hayo Bofya hapa..........

KIONGOZI WA TALIBAN PAKISTAN ARIPOTIWA KUUAWA NAO WACHAGUA KIONGOZI MPYA

Kiongozi nambari mbili wa kundi la Taliban nchini Pakistan Waliur Rahman ameuawa katika mashambulizi ya ndege zisizo na rubani za Marekani katika eneo la Waziristan. Maafisa Usalama wa Pakistan wametangaza kuwa, Waliur Rahman ambaye Marekani ilitangaza zawadi ya dola milioni 5 kwa kichwa chake, ameuawa pamoja na wafuasi wake wasiopungua watano baada ya makombora mawili kulenga nyumba yake mapema hapo jana.
Hata hivyo msemaji wa kundi la Taliban amekanusha taarifa hizo na kusema kuwa si za kweli. Kundi la Taliban la Pakistan ni kundi tofauti lakini lenye mfungamano na kundi la Taliban wa Afghanistan na linajulikana kwa jina la Tahreek-e- Taliban Pakistan (TTP). Kundi hilo limefanya mashambulizi mengi dhidi ya jeshi la Pakistan na raia wasio na hatia nchini humo.

MAKAAZI MAPYA YA WALOWEZI YATATIZA AMANI PALESTINA

Mpatanishi mkuu wa Palestina Saeb Erakat amesema kuwa uamuzi wa Israel wa kujenga makaazi mapya ya walowezi wa kiyahudi mashariki mwa Jerusalem unaharibu juhudi za Marekani za kufufua mazungumzo ya kutafuta amani kati ya nchi hizo mbili.Erakat amesema wanauchukulia uamuzi huo wa Israel wa kujenga makaazi mengine 1,000 kama hatua ya kuhujumu juhudi za waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry.Matamshi ya Erakat yanawadia saa chache baada ya shirika lisilokuwa la serikali kuliambia shirika la habari la AFP kuwa Israel inapanga kujenga makaazi zaidi mjini Jerusalem huku Marekani ikijizatiti kuyafufua mazungumzo yaliyokwama kati ya Palestina na Israel.Ujenzi huo wa makaazi ya walowezi umekuwa ndilo suala  tete lililosababisha kufeli kwa mazungumzo mwaka 2010 na wapalestina wameapa kutorejea katika meza ya mazungumzo iwapo Israeli itaendelea kujenga katika ardhi yao.

WAPINZANI SYRIA KUTOSHIRIKI MAZUNGUMZO YA AMANI

Muungano wa kitaifa wa upinzani Syria umesema hautashiriki katika mazungumzo yanayoandaliwa kwa pamoja na Urusi na Marekani huku washirika wa utawala wa Rais wa Syria Bashar al Assad ukijihusisha katika vita kwa kulisaidia jeshi la serikali.Kaimu kiongozi wa muungano huo  George Sabra amewaambia waandishi habari mjini Istanbul Uturuki kuwa muungano huo hautashiriki katika mkutano wowote wa kimataifa au katika juhudi zozote za amani iwapo wapiganaji kutoka Iran na wa kundi la wanamgambo la Hezbollah kutoka Lebanon wataendelea kuivamia Syria.
Wakati huo huo waasi wameomba msaada wa klijeshi na madawa katika mji wa mpakani wa Qusair ambako mapigano makali na majeshi ya serikali yanaendelea. Msemaji wa waasi amesema kuna majeruhi 700 mjini humo.Majeshi ya Assad yanasemekana yanasonga mbele kuuteka mji wa Qusair wakisaidiwa na wapiganaji wa Hezbollah kutoka Lebanon.

WHO YATAKA KUPIGWA MARUFUKU MATANGAZO YA SIGARA

Shirika la Afya Duniani WHO limetaka mataifa yote duniani kupiga marufuku matangazo yote ya biashara ya tumbaku kama njia mojawapo ya kupunguza idadi ya wavutaji wapya wa tumbaku. Katika taarifa, WHO inasema kuwa nchi ambazo tayari zimetekeleza marufuku ya matangazo na udhamini kwa bidhaa za tumbaku zimeshuhudia kupungua kwa matumizi ya tumbaku kwa asilimia saba. Nchi ambazo zimepiga marufuku matangazo ya bidhaa za tumbaku ni pamoja na Australia, Canada, Finland, Ireland, Nepal, New Zealand, Norway, Palau na Panama. Kabla ya maadhimisho ya siku ya kupinga matumzi ya tumbaku duniani ambayo ni tarehe 31 mwezi huu, WHO inasema kuwa sekta ya tumbaku inatafuta mbinu tofauti za kulenga wavutaji sigara kupitia mitandao ya mawasiliano au kwa kutumia wafanyikazi wa makampuni ya tumbaku wanaojifanya kuwa wavutaji sigara. Dr Douglas Bettcher mkurugenzi katika idara ya kuzuia magonjwa yasiyoambukiza kwenye Shirika la WHO amesema marufuku kwa aina  zote za matanagazo na udhamini  ni moja ya njia kuu ya kupunguza matumizi ya tumbaku. Amesema watumiaji wengi wa tumbaku huanaza kuitumia kabla ya kutimia miaka 20 na hakuna shaka kuwa sigara ni mada inayoua na kwamba njia pekee ni kupigwa marufuku matangazo yote ya biashara na udhamini wa bidhaa hiyo.

WAGOMBEA URAIS IRAN KUANZA MDAHALO KESHO

Mdahalo wa kwanza wa televisheni kati ya wagombea wanane wa duru ya 11 uchaguzi wa rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran utafanyika kesho Ijumaa na kurushwa hewani moja kwa moja na kanali ya kwanza ya televisheni. Mdahalo huo wa kwanza utafanyika saa 10 jioni kwa majira ya hapa nchini na kuwashirikisha wagombea wote wanane wa kiti cha urais. Mdahalo huo utarushwa hewani tena saa tatu usiku hapo kesho katika kanali ya nne ya televisheni. Mbalo na mdahalo wa kesho, wagombea katika uchaguzi wa rais wa Iran watachuana tena katika midahalo mingine miwili itakayofanyika siku ya Jumatano ya tarehe 5 na siku ya Ijumaa ya tarehe 7 Juni. Duru ya 11 ya uchaguzi wa rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pamoja na uchaguzi wa nne wa mabaraza ya Kiislamu ya miji na vijiji zitafanyika kwa wakati mmoja siku ya Ijumaa ya tarehe 14 Juni

MECHI KATI YA WANAFUNZI WA MUHIMBILI NA CHUO CHA DIT.


Jumuiya ya wanafunzi wa kiislam wa Muhimbili inawaalika waislam na wanafunzi wengine wa Muhimbili kuhudhuria Mpambano Mkali wa kabumbu katika wanafunzi wa Muhimbili na kutoka chuo cha DIT.  Eneo ni uwanja wa Muhimbili nyuma ya Jengo la Mwaisela, au moja kwa moja ukiingilia geti la Chuo.

Kiingilio ni macho yako kwani ni mechi ya kuimarisha Udugu na timu ya Muhimbili imedhamiria kurudisha heshima ya kufungwa mara mbili na DIT katika mechi ya kwanza iliyofanyika Muhimbili na ya Marudiano ambayo ilifanyika huko DIT.

Wote Munaalikwa kuja kufurahi na kupunguza Mawazo.

HALI YA WAISLAMU MYANMMAR BADO TETE, WAENDELEA KUUWAWA

Mwislamu moja ameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya katika hujuma mpya ya Mabudha wenye misimamo mikali dhidi ya Waislamu nchini Myanmar.Katika hujuma ya Jumanne, Mabudha waliteketeza kwa moto mali za Waislamu katika mji wa Lashio kaskazini mashariki mwa Myanmar. Kati ya sehemu zilizoteketezwa katika hujuma ya mamia ya Mabudha ni msikiti mkubwa na makao ya mayatima.  Machafuko hayo yametilia shaka madai ya serikali ya Rais Thein Sein wa Myanmar kuwa anataka kumaliza hujuma dhidi ya Waislamu waliowachache nchini humo. Karibu Waislamu 800,000 wa kabila la Rohingya nchini Myanmar wamekuwa wakikandamizwa na Mabudha wenye misimamo ya kufurutu mipaka. Mabudha hao wameteketeza kwa moto vijiji na misikiti ya Waislamu. Aidha serikali ya Myanmar inatuhumiwa kuwa imekataa makusudi kuwasaidia Waislamu hao walio wachache nchini humo. Maelfu ya Waislamu wa kabila la Rohingya wameuawa na makumi ya maelfu ya wengine kuachwa bila makao katika miezi ya hivi karibuni.

WHO: PIGENI MARUFUKU MATANGAZO YA TUMBAKU KULINDA VIJANA

Shirika la afya duniani (WHO) linazitaka nchi zote duniani kupiga marufuku ya matangazo ya tumbaku ikiwemo kutokudhamini ili kulinda afya za wanadamu hasa vijana ili kupunguza idadi ya watumiaji wa bidhaa hiyo. Kupiga marufuku huko kutapunguza idadi ya vifo duniani kwani kila mwaka watu milioni 6 hufa kutokana na madhara ya tumbaku. Pia watu laki 6 amabo sio watumiaji hufa kutokana na madhara wayapatayo kutokana na moshi wa tumbaku kutoka kwa watumiaji. Nchi zilizopiga marufuku tayari zimeshashuhudia upungufu wa matumizi ya tumbaku kwa asilimia 7. Mpaka kufikia 2030 utafiti unaonesha kuwa vifo vitaongezeka kutoka milioni 6 kwa mwaka mpaka 8 ikiwa juhudi za haraka hazitochukuliwa. Dr Douglas Bettcher anasema "watumiaji wengi wa tumbaku huanza utegemezi mkubwa wa bidhaa hiyo kabla ya miaka 20" Pia Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Dr Margaret Chan anasema kuwa Nchi zote ni lazima zitoe kipaombele katika kudhibiti viwanda vya tumbaku visivyo na aibu katika kutengeneza matangazo yanayovutia yanayowarubuni hasa vijana wengi na wanawake na hatimaye kutengeneza kizazi kilichoathirika na matumizi ya nikotini.

SYRIA YAPATA ZANA MPYA ZA MPYA ZA KIVITA KUTOKEA URUSI

Syria imepokea zana za kisasa za kivita kutokea Urusi. Zana hizo zijulikanazo kwa jina la S-300 zina uwezo wa kuzuia makombora ya angani na ya ardhini. Maelezo hayo yametolewa na Rais Bashar Al-Assad. Rais huyo amedai kuwa ndo kwanza pamekucha na vita bado Mbichi na ndo inaanza kushika kasi. Aliyasema hayo kupitia kituo cha televisheni chenye mahusiano ya kikundi cha Hizbollah. Urusi imeahidi kuendelea kuihami Syria baada ya nchi hiyo kuondolewa vikwazo vya silaha. Wachambuzi wa mambo wanadai huenda nchi zinazojihusisha na mgogoro huu zikaanza kutumia silaha zake hasa baada ya Syria kusema kuwa ipo tayari kujibu mashambulizi yoyote na kulipiza kisasi dhidi ya Israel.Nae waziri wa mambo ya ndani wa Syria amesema sasa jeshi la Syria limerudi katika hali bora ya kupambana na waasi.

VIRUSI VIPYA VILIVYOGUNDULIKA VYAZIDI KUUWA WATU MASHARIKI YA KATI

Taarifa zilizotolewa na shirika la afya duniani (WHO) zinasema kuwa wagonjwa 27 kati ya 49 waliogundulika na virusi hivyo, wameshafariki dunia. Sirika hilo sasa limetangaza kuwa virusi hivyo ni hatari kwa dunia kwani vinazidi kusambaa hivyo nchi zinatakiwa kuwa makini hasa kwa wasafiri wanaotembelea baadhi ya nchi za kiarabu kama Saudi Arabia, Falme za Kiarabu (UAE), Jordan na Qatar. Pia baadhi ya wagonjwa wamepatikana Ufaransa, Tunisia, Uingereza na Ujerumani. Vifo vya hivi karibuni vimetokea mashariki mwa nchi ya Saudi Arabia ambapo watu watatu wamefariki kutokana na virusi hivyo. Pia mgonjwa mmoja alifariki dunia huko Ufaransa baada ya kutokea Mashariki ya kati. Wataalamu wanadai virusi hivyo sio SARS (Severe Acute Respiratory Syndrome) bali ni virusi vipya ambavyo wao wamevipa jina la MERS-CoV (Middle East Respiratory Syndrome Coronavirus). Dalili za ugonjwa huo ni pamoja na kuhisi baridi kali ambayo inapelekea kupata nimonia na pia figo kutofanya kazi ipasavyo. Shirika hilo la afya limomba wataalamu wote duniani kushirikiana nao na kufanya utafiti wa hali ya juu ili kuweza kuzuia virusi hivi visiendelee kuenea na kusababisha vifo vya watu wengi duniani. 

MSIBA MKUBWA: NDOA YA KWANZA YA JINSIA MOJA YAFUNGWA NCHINI UFARANSA


Baada ya sheria ya ndoa za jinsia moja kuhalalishwa nchini Ufaransa, ndoa ya kwanza yafungwa jana huko Montpellier, Ufaransa. Wakionekana kufurahia ndoa yao, Bwana Bruno Boileau anaeleza kuwa ana furaha kubwa kwa kufanikiwa kwa ndoa hiyo. Anaeleza sababu za kumpenda mwanaume mwenzake ambae kwa sasa ndio "Mke wake" aitwae Vincent Autin kwa ni mtu aneweza kumtuliza, mwenye mvuto, anayejitambua na mwenye matarajio makubwa. Nae bwana Vincent asema anampenda "Mume wake" kwasababu anamlinda vizuri na ndio mlinzi wake anaemtegemea. Bruno anasema kwa kujiamini, "tunataka tupate watoto na tunataka tuendeleze mila hii mpaka vizazi vijavyo". Nae Vincent anasema "Ufaransa leo imeturudishia haki yetu ya msingi ambayo tumezaliwa nayo". Na hapa ndipo ulimwengu ulipofikia, sijui huko tunakoelekea itakuaje???? 


Tuesday, May 28, 2013

CHINA YAKANUSHA WIZI WA TAARIFA ZAMTANDAO ZA SHIRIKA LA KIJASUSI LA AUSTRALIA

Serikali ya Australia imeituhumu nchi ya China kwa kuhusika na wizi wa taarifa za siri toka shirika lake la kijasusi, waziri wa mambo ya kigeni wa Australia, Bob Carr amedhibitisha. Kwenye taarifa yake, waziri Carr amesema kuwa kufuatia uchunguzi walioufanya wamebaini kuwa maharamia waliovamia mtandao wa shirika la ujasusi wa nchi hiyo walitokea nchini China ambapo wamefanikiwa kuiba baadhi ya nyaraka na programu za vitarakilishi.
Waziri Carr ameongeza kuwa licha ya taarifa hiyo uhusiano baina ya mataifa hayo mawili utaendelea kusalia kama kawaida wakati huu ambapo wakifanyia kazi suala hilo ikiwemo kubaini waliohusika na uharamia. Tukio hili linatokea ikiwe umepita mwezi mmoja toka ikulu ya Marekani iituhumu nchini ya China kuhusika na wizi wa taarifa za Serikali yake tuhuma ambazo China imekanusha.
Tayari wizara ya mambo ya kigeni ya China imekanusha nchi yake kuhusika moja kwa moja na wizi wa taarifa za siri nchini Australia na Marekani na kwamba wanaofanya hivyo ni kikundi cha maharamia wachache walioko nchini mwake. Wataalamu wa masuala ya mtandao wanasema kuwa ni vigumu sana kwa sasa kuwabaini maharamia waliotekeleza wizi huo.

RAIS WA SUDAN ATISHIA KULIFUNGA BOMBA LA MAFUTA TOKA KUSINI

Rais wa Sudan, Omar al-Bashir ametishia nchi yake kulifunga kabisa bomba lake la mafuta linalotoka nchini Sudan Kusini kuelekea kwenye pwani ya bahari ya Khartoum iwapo nchi hiyo haitaacha kuwaunga mkono waasi wa Sudan. Akizungumza kupitia njia ya Televisheni, rais Bashir amesema kuwa Serikali yake italifunga bomba hilo la mafuta iwapo serikali ya Juba itaendelea kuwaunga mkono waasi wanaopigana kwenye jimbo la Darfur wakilenga kumpindua. Rais Bashir amesema kuwa hili ni onyo lake la mwisho kwa Serikali ya Juba na kwamba italifunga kabisa bomba hilo iwapo Juba itaendelea kushirikiana na waasi wa Darfur, Kordofan Kusini na Blue Nile ambao wamekuwa wakipigana na Serikali.
Kundi la waasi wa SRF wameanzisha mashambulizi mapya kwenye baadhi ya maeneo nchini Sudan na sasa wanaumiliki mji wa Um Rawaba ulioko katikati mwa nchi hiyo. Hivi karibuni pia kundi la SPLM-North lilitangaza kujiunga na waasi wa Darfur, JEM na wale waliojitenga kutoka jeshi la Sudan SLA ambao waliunda kundi la Sudan Revolutionary Front SRF mwishoni mwa mwaka jana.
Toka nchi ya Sudan Kusini kujitenga na Sudan kati kati ya mwaka 2011 nchi hizo zimekuwa zikivutana kuhusu uzalishaji wa mafuta na kugombea mpaka jambo ambalo mara kadhaa lilisababisha nchi hizo kutumbukia kwenye vita. Serikali ya Juba imekanusha kushirikiana na makundi ya waasi wa Darfur wanaopigana nchini Sudan na kwamba yenyewe inapambana na waasi ambao wanaendesha mashambulizi kwenye jimbo la Jonglei.

MIRIPUKO 21 YA MABOMU IRAQ YAUA 176

Watu wasiopungua 176 wameuawa na kujeruhiwa baada ya kujiri milipuko 21 ambapo 17 kati ya hiyo ilikuwa ya utegaji mabomu ndani ya magari kwenye maeneo mbalimbali huko Baghdad mji mkuu wa Iraq. Taarifa zinasema kuwa, watu wasiopungua 85 wameuawa na wengine wasiopungua 90 kujeruhiwa kwenye milipuko hiyo iliyotokea ndani ya muda wa masaa mawili tu mjini Baghdad. Milipuko hiyo imetokea katika hali ambayo, majeshi ya ardhini na angani ya nchi hiyo siku ya Jumapili yalitekeleza oparesheni kubwa  katika mikoa ya al Anbar ulioko magharibi, Babil ulioko katikati,  Karkuk ulioko kaskazini  na mkoa wa Diyala ulioko mashariki mwa Iraq na kufanikiwa kuwaangamiza magaidi 14 na kuwakamata wengine 76.

WAFADHILI WA WAASI WA SYRIA WAKIRI JESHI LINA UWEZO MKUBWA

Nchi nyingi zinazowaunga mkono kifedha na kisilaha waasi wa Syria, zimekiri uwezo mkubwa na jeshi la nchi hiyo na kushindwa waasi katika medani ya mapambano. Mtandao wa Intaneti wa gazeti la al-Manar linalochapishwa Baytul Muqaddas umeandika kuwa, nchi nyingi ambazo hadi sasa zinawapa misaada waasi nchini Syria, zimetambua kwamba, waasi hao hawana uwezo wa kuunganisha nguvu zao wala kufikia mwafaka wa pamoja hasa katika kutafuta njia mbadala itakayoweza kuangusha serikali hahali ya Rais Bashar al-Assad wa nchi hiyo. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, licha ya waasi hao kukosa makubaliano kati yao, wameshindwa pia katika uwanja wa mapambano na hivyo kushindwa kabisa kuchukua maamuzi yoyote kuhusu mustakbali wa nchi hiyo. Kwa upande mwingine, magaidi hao wamezidi kuchukiwa vikali katika jamii ya Syria, kutokana na jinai za kutisha walizozifanya dhidi ya raia wa nchi hiyo. Asilimia kubwa ya Wasyria wanaamini kuwa, waasi hao wanaooungwa mkono kutoka nje, ndio chanzo kikuu cha mgogoro na machafuko nchini mwao.

WAKIMBIZI LAKI NNE WA MALI WANA HALI MBAYA

Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu nchini Mali limetangaza kuwa, tangu mwezi Januari mwaka jana hadi sasa, karibu raia laki nne wa nchi hiyo, wamelazimika kukimbilia maeneo yenye amani baada ya maeneo yao kukumbwa na machafuko. Mkurugenzi wa Shirika hilo PeterMoorer amewambia waandishi wa habari kuwa, karibu raia wa Mali wapatao laki nne, ni wakimbizi wa ndani ya nchi yao. Ameongeza kuwa, wakimbizi hao wanaishi katika kambi za wakimbizi huku wengine wakilazimika kuishi kwa ndugu zao. Amesema kuwa wale ambao ndugu zao hawana uwezo wa kifedha wanaishi hali mbaya sana ya kibinaadamu. Moorer amesisitiza kuwa, Shirika la Msalaba Mwekundu, limekuwa likishindwa kufikisha misaada kwa wakimbizi hao, kutokana na sababu za ukosefu wa usalama, uthabiti na kuongezeka vitendo vya utumiaji mabavu katika maeneo ya kaskazini mwa Mali. Aidha amesema kuwa, ukiachilia mbali idadi hiyo ya wakimbizi wa ndani, idadi kubwa nyingine ya wakimbizi wa nchi hiyo, wamekimbilia nchi za jirani zikiwemo za Mauritania, Niger, Burkina Faso na Algeria.

WAISLAM LAGOS WAPINGA MARUFUKU YA KUVAA HIJAB NIGERIA

Wakazi wa mjini Lagos, Nigeria, wameendelea kulalamikia marufuku ya vazi takatifu la Kiislamu yaani Hijab katika shule za serikali za mjini huo. Habari zaidi zinasema kuwa, jana mitaa yote iliyo karibu na Mahakama Kuu ya mjini Lagos, ilishuhudia maandamano makubwa ya Waislamu wa mji huo wakipinga marufuku hiyo, waliyoitaja kuwa ni mwanzo wa kukanyagwa haki za Waislamu nchini Nigeria. Hivi karibuni serikali ya Abuja ilitangaza marufuku ya kuvaa Hijab katika shule za serikali za mjini Lagos. Wakati huo huo Mahakama Kuu ya mjini hapo imesema kuwa, itachunguza ombi la Waislamu, waliotaka kuondolewa marufuku hiyo mara moja. Aidha Nigeria ina jumla ya raia milioni 170 ambapo karibu nusu ya idadi hiyo inaundwa na Waislamu nchini humo.

Monday, May 27, 2013

TAHARUKI MPAKANI MWA LEBANON NA ISRAEL

Wanajeshi wa Israel wanafanya msako katika mpaka wake wa Kaskazini kufuatia ripoti za mashambulizi ya roketi zinazorushwa kutoka Kusini mwa Lebanon. Shirika la habari la Lebanon limesema kuwa makombora ya roketi yamerushwa nchini Israeli kutoka kusini mwa Lebanon. Haijafahamika wazi ni nani aliyefyatua makombora hayo na ni wapi yaliangukia . Jeshi la Israel linasema linachunguza taarifa hizo. Tukio hilo limetokea wakati hali ya wasi wasi ikitanda katika kanda hiyo kufuatia vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea nchini Syria .
Televisheni ya kundi la Hezbollah ya al-Manar imesema roketi ilirushwa ndani ya Israil usiku wa kuamia leo na kulenga mji wa kusini wa Israil unaojulikana kama Metulla. Wakaazi wa mji huo wanasema walisikia mlipuko lakini hakuna ripoti kuhusu watu kujeruhiwa au kuuawa. Televisheni hiyo inasema kikosi cha ulinzi cha Israil kilipelekwa katika eneo la mpakani na hadi sasa hakujatokea mashambulio yoyote. Bado haijulikani ni nani alirusha roketi hiyo.
Wachambuzi wa maswala ya usalama wanasema kuna uwezekano kuwa kundi la Hezbollah halikuhusika na huenda waliotekeleza shambulio hilo walitaka kuchochea mzozo kati ya Israil na kundi hilo.

MAWAZIRI WA UMOJA WA ULAYA WAGAWANYIKA JUU YA SUALA LA SYRIA

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya EU wamegawanyika kuhusu mpango wa kuwaondolea vikwazo vya silaha waasi wa Syria au la, wakati huu ambapo muda makataa hiyo unafikia tamati. Licha ya mgawanyiko kushuhudiwa ndani ya mkutano ulioanza hii leo mjini Brussels Ubelgiji, mkuu wa sera za mambo ya nje wa Ulaya EU, Catherine Ashton amesema kuwa kuna matumaini makubwa ya viongozi hao kufikia muafaka. Mgawanyiko huo umedhibitishwa na waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Guido Westerwelle ambaye amekiri kuwa nchi nyingi za Umoja huo bado hazijaonesha wazi msimamo wao kuhusu kuwaondolea vikwazo waasi au la.
Mgawanyiko huo unatokana na hofu ya kwamba huenda mashambulizi ya mabomu ya kujitoa muhanga yanayotekelezwa nchini humo unatokana na uzagaaji wa silaha kwa upande wa waasi ambao wanatuhumiwa kushirikiana na makundi ya kigaidi nchini Syria. Hofu hiyo pia inazidi kufuatia madai ya Urusi na China kuwa waasi wa Syria wamekuwa na uhusiano na makundi ya kigaidi ambayo yanahatarisha usalama wa nchi hiyo kwakuwa silaha nyingi ziko mikononi mwa waasi. Marekani ambayo ni mshirika mkubwa kutaka kuhakikisha silaha zinatolewa kwa waasi pia imeonesha hofu yake na kudai kuwa inafikiria upya suala la kuwaondolea makataa ya silaha upande wa waasi.
Miongoni mwa nchi zinazounga mkono mkakati huo ni pamoja na Uturuki, Uingereza na Ufaransa ambazo zilikiri wazi kuwasaidia waasi kwa silaha. Kumekuwa na mazungumzo tofauti juma hili kujaribu kumaliza mzozo wa Syria huku waasi wenyewe nao wakigawanyika kuhusu uwepo wa Serikali ya Assad kwenye mazungumzo ya Geneva.

HOTUBA YA KIONGOZI WA HIZBULLAH JUU YA USHINDI WAO DHIDI YA ISRAEL

Tarehe 25 Mei inasadifiana na kumbukumbu ya ushindi wa muqawama dhidi ya Wazayuni na kukombolewa maeneo ya kusini mwa Lebanon. Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya nchini Lebanon Hizbullah Sayyid Hassan Nasrullah amehutubia kumbukumbu hizo na kugusia mambo mengi. Sayyid Hassan Nasrullah ameitaja siku ya kukimbia kwa madhila askari vamizi wa Kizayuni katika maeneo ya kusini mwa Lebanon kuwa ni 'Siku ya Mwenyezi Mungu' na kuongeza kuwa, ushindi huo si kwa ajili ya Walebanoni peke yao, bali ni kwa ajili ya mataifa yote ya Waislamu wote duniani. Amefafanua kuwa, ushindi huo ulifikiwa kutokana na juhudi za kila aliyetoa mchango wake katika mapambano ya kuwang'oa Wazayuni nchini bali na si ushindi wa Hizbullah pekee. Hata hivyo yapo baadhi ya makundi nchini Lebanon, baada ya kushindwa kuipokonya silaha Harakati hiyo ya Hizbullah, sasa yanafanya njama nyingine za kuvunja kabisa harakati ya muqawama nchini humo. Vile vile amesema, hivi sasa Lebanon ina serikali dhaifu kiasi kwamba haiwezi hata kutatua mambo yake ya ndani kama vile kufikia mwafaka kuhusu sheria ya uchaguzi. Kwa mara nyingine amesisitiza kuwa, silaha za harakati ya muqawama zinatumika tu katika mapambano na Wazayuni na zitaendelea kupata uungaji mkono wa wananchi wa taifa hilo la Kiarabu. Aidha Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya nchini Lebanon Hizbullah ameashiria kwamba, baadhi ya nchi zinafanya njama kubwa za kuliweka jina la harakati hiyo katika orodha ya makundi ya kigaidi na kusisitiza kuwa, njama hizo hazina taathira yoyote kwa Harakati ya Hizbullah. Amesema, suala la kuliweka jina la Hizbullah katika orodha ya makundi ya kigaidi duniani, itabakia kuwa wino tu juu ya karatasi, kwani harakati hiyo itaendelea na muqawama wake dhidi ya adui Mzayuni. Katika sehemu nyingine ya hotuba yake Sayyid Hassan Nasrullah ameashiria njama za baadhi ya mirengo ndani na nje ya Lebanon za kuvuruga hali ya usalama mjini Tripoli kaskazini mwa nchi hiyo na kusema kuwa, machafuko ya mjini Tripoli lazima yakomeshwe kwa thamani yoyote iwayo. Alisema jeshi la Lebanon pekee ndilo lenye dhamana ya kulinda usalama ndani ya nchi hiyo hususan katika keneo hilo. Aidha ameashiria hujuma za kila namna za mabeberu wanaopenda kujitanua wakiongozwa na Marekani wakishirikiana na baadhi ya tawala za kidikteta za Kiarabu pamoja na Uturuki dhidi ya taifa la Syria na kuzionya vikali nchi za eneo hili kutokana na hatari kubwa ya makundi ya Kiwahabi yenye misimamo mikali inayokufurisha Waislamu wengine. Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya nchini Lebanon Hizbullah pia amesema, kile kinachojiri hivi sasa nchini Syria, ni matokeo ya uungaji mkono wa baadhi ya nchi za Kiarabu kwa makundi ya kigaidi. Alisema nchi hizo zinawatuma Mawahabi hao wenye misimamo mikali nchini Syria, ili zenyewe ziweze kuepukana na shari ya makundi hayo na wakati huo huo ziweze pia kuiangusha serikali halali ya Damascus. Sayyid Hassan Nasrullah amesema kama ninavyomnukuu: "Hivi sasa ulimwengu wa Kiislamu na Waislamu wako katika kipindi nyeti sana cha historia na haifai kupoteza muda kwani umefika wakati wa kusimama kidete kukabiliana na kimbunga hiki." Mwisho wa kunukuu. Amesema, machafuko ya nchini Syria ni kwa manufaa ya utawala haramu wa Kizayuni na ni hatari kubwa kwa nchi za eneo la Mashariki ya Kati na umma mzima wa Kiislamu.

WAHAFIDHINA WAPINGA UJENZI WA MSIKITI ATHENS

Chama cha kihafidhina cha Golden Dawn nchini Ugiriki kwa mara nyingine tena kimeupinga mpango wa serikali ya nchi hiyo wa kujenga Msikiti katika mji mkuu wa nchi hiyo Athens. Ilias Kasidiaris msemaji wa chama hicho cha kihafidhina amewaambia waandishi wa habari mjini Athens kwamba iwapo serikali ya nchi hiyo haitaachana na mpango wa kujenga Msikiti huo, chama hicho kitawakusanya wafuasi wake zaidi ya laki moja na kuzuia ujenzi wa msikiti huo. Taarifa kutoka Athens zinasema kuwa, wafuasi wa chama hicho wamewaonya Waislamu wafute wazo la kujengwa msikiti mjini humo, la sivyo watachinjwa kama kuku. Taarifa zinasema kuwa, Athens ndio mji mkuu pekee barani Ulaya ambao hadi sasa hakuna hata msikiti mmoja. Imeelezwa kuwa, idadi ya Waislamu nchini Ugiriki inafikia laki tatu, na serikali ya Ugiriki imekubali matakwa ya Waislamu ya kujengwa Msikiti katika eneo ambalo awali kulikuwa na kambi ya kijeshi ya nchi hiyo. Baadhi ya viongozi wa Kanisa la Orthodox na chama cha Golden Dawn wanadai kuwa, ujenzi wa msikiti huo utasababisha kupotea utambulisho wa Kikristo nchini humo. Amma serikali ya Ugiriki imesisitiza mpango wake wa kujenga msikiti katika mji mkuu wa nchi hiyo hata kama kuna upinzani wa mirengo ya wahafidhina nchini humo. Waislamu wengi wanaoishi nchini humo wanatoka nchi za kaskazini mwa Afrika, Mashariki ya Kati na kusini mwa Asia.

JENERALI SEJUSA AOMBA ULINZI UINGEREZA

Jenerali wa jeshi la Uganda anayetafutwa na serikali ya nchi hiyo ameomba ulinzi wa polisi ya Uingereza na hatorudi nyumbani hivi karibuni. Joseph Luzige, wakili wa Jenerali David Sejusa, amesema Jenerali huyo hivi sasa amekuwa akijificha kuwakimbia makachero wa Uganda ambao inadaiwa kuwa wametumwa kwenda kumsaka akiwa safarini huko London Uingereza. Wakili huyo amesema Sejusa anayeongaza idara za usalama za ndani na nje ya Uganda anaamini kwamba maisha yake yako hatarini na kwamba amekuwa muangalifu sana. Hivi karibuni, jenerali huyo aliandika barua kwa idara ya usalama ndani ya nchi kutaka ufanyike uchunguzi juu ya repoti kuhusu mpango wa kumrithisha madaraka mtoto wa kiume wa Rais Yoweri Museveni ambapo wale wanaoupinga mpango huo wako katika hatari ya kuuwawa.

UJERUMANI YAVUNJA REKODI YA KUUZA SILAHA NDOGONDOGO

Mauzo ya silaha ndogo ndogo za Ujerumani ya mwaka jana yanaripotiwa kuvunja rikodi ambayo haikuwahi kushuhudiwa hapo kabla. Kampuni za kutengeneza silaha za Ujerumani zimejipatia mapato makubwa zaidi hapo mwaka 2012 kutokana na mauzo ya silaha ndogo ndogo kuliko mwaka 2011 kwa mujibu wa Südeutscghe Zeitung. Kwa mujibu wa gazeti hilo mauzo ya silaha hizo zilizosafirishwa nje kwa mwaka 2012 yamefikia euro milioni 76.15 kulinganisha na euro milioni 37.9 kwa mwaka 2011. Kiwango kikubwa cha mauzo hayo kuwahi kurikodiwa katika ripoti ya serikali ya Ujerumani ya mauzo ya silaha ndogo nje ya nchi tokea mwishoni mwa miaka 1990, ilikuwa kuanzia mwaka 2009 ambapo yalifikia euro milioni 70.4. Gazeti hilo limesema limepata takwimu hizo kutoka kwa chama cha Linke cha sera za mrengo wa shoto. Bastola,bunduki nyepesi za rashasha,mabomu madogo kama yale yanayaoweza kurushwa kwa mkono na mabomu ya kutegwa ardhini ni miongoni mwa silaha zinazohesabiwa kuwa ndogo.

SERBIA NA KOSOVO WARIDHIA MAHUSIANO

Umoja wa Ulaya leo umekaribisha idhini ya uhakika iliyotolewa na Serbia na Kosovo kurudisha uhusiano wao katika hali ya kawaida na kusema kwamba hiyo ni hatua moja mbele katika juhudi za kujiunga na Umoja wa Ulaya.
Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja huo, Catherine Ashton, amesema anakaribisha uamuzi wa nchi hizo mbili kuupitisha mpango wa utekelezaji ambao unatafsiri kwa vitendo vifungu vya makubaliano waliofikia hapo mwezi wa Aprili. Serikali ya Kosovo iliuidhinisha kwa haraka mpango huo wa utekelezaji baada ya Waziri Mkuu wa Serbia, Ivica Dacic, na mwenzake wa Kosovo, Hashim Thaci, kuufafanuwa hapo Jumatano. Serikali ya Serbia hadi jana usiku ilikuwa ikiutafakari kwa kutaka hakikisho kwamba idhini ya kuutekeleza mpango huo wenye nia ya kurudisha maisha yaliyochafuliwa kutokana na mzozo huko Kosovo hapo mwaka 1999 katika hali ya kawaida, haitomaanisha kwamba serikali hiyo inatambuwa uhuru wa jimbo lake hilo lililojitenga.

JESHI LA SUDAN LAANGAMIZA WAASI 70

Jeshi la Sudan limetangaza kuwa, kwa akali waasi 70 wameangamizwa katika eneo la al Dandaro lililoko katika jimbo la Kordofan Kusini. Kanali al Sawarmy Khalid Saad Msemaji wa jeshi la Sudan amesema kuwa, kundi hilo la waasi likitumia silaha nzito kama vile vifaru na mizinga lilivamia eneo la al Dandaro lililoko katika jimbo hilo kwa shabaha ya kulidhibiti, lakini lilikumbana na upinzani mkali kutoka kwa majeshi ya serikali ya Khartoum. Kanali Khalid Saad ameongeza kuwa, kwenye mapigano hayo waasi wasiopungua 70 waliuawa na wengine kukimbia baada ya kuzidiwa nguvu na majeshi ya serikali ya Sudan. Amesema kuwa, majeshi ya serikali yamefanikiwa kukamata ngawira za vifaru viwili aina ya T55 na zana nyingine za kijeshi za waasi.

WAFANYABIASHARA WA JORDAN WASUSIA KIKAO NA UJUMBE WA ISRAEL

Wafanyabiashara wa Jordan wamesusa na kutoka nje ya kikao cha Jukwaa la Kimataifa la Uchumi 'Davos' nchini Jordan, mara baada ya kuingia kwenye kikao hicho ujumbe wa utawala wa Kizayuni. Hatua ya wafanyabiashara wa Jordan inaonyesha msimamo wa nchi hiyo wa kulalamikia vitendo vinavyoyadhalilisha matukufu ya Kiislamu vinavyofanywa na utawala huo ghasibu. Wiki iliyopita, serikali ya Jordan ilimfukuza balozi wa utawala wa Israel mjini Amman ikilalamikia hatua ya kuvunjiwa heshima Masjidul Aqswa, kibla cha kwanza cha Waislamu. Serikali ya Jordan ilichukua hatua hiyo baada ya wabunge wa nchi hiyo kutoa mashinikizo makubwa ya kuitaka serikali imfukuze balozi wa utawala wa Israel nchini humo.

WAANDAMANAJI WAPINGA NDOA YA JINSIA MOJA UFARANSA

Mamia ya maelfu ya wananchi wa Ufaransa walifanya maandamano makubwa mjini Paris hapo jana wakipinga kupitishwa sheria mpya ya ndoa ya watu wa jinsia moja nchini humo. Waandamanaji hao wameonyesha hasira zao kwa kupinga kitendo hicho cha kinyama kinachokinzana na maadili ya mwanadamu na kuitaka serikali ya nchi hiyo iitengue mara moja. Waandamanaji wameahidi kuendelea kutoa mashinikizo yao hadi pale serikali ya Rais Francois Hollande itakaposalimu amri. Wanaharakati wa kijamii wameeleza kuwa, watu wanaokaribia milioni moja wameshiriki kwenye maandamano hayo ya amani yanayopinga kupitishwa sheria ya ndoa ya watu wa jinsia moja ambayo imeanza kutekelezwa tokea wiki iliyopita. Inafaa kuashiria hapa kuwa, siku chache zilizopita mwandishi mmoja wa Kifaransa alijinyonga Kanisani nchini Ufaransa akipinga kupitishwa sheria hiyo nchini humo.

AL SHABAB WAZIDISHA MASHAMBULIZI NDANI YA KENYA

Watu wanane wameuawa baada ya wanamgambo wa kundi al al Shabab kufanya mashambulizi ndani ya ardhi ya Kenya. Sheikh Abdi Aziz abu Mas'ab Msemaji wa kundi la al Shabab amesema kuwa, kundi hilo limefanikiwa kuwauwa watu wanane baada ya kushambulia makao ya kijeshi katika eneo la Damajale nchini Kenya. Msemaji wa al Shabab ameongeza kuwa, kwenye shambulizi hilo, wanamgambo wa al shabab wamewateka nyara wanajeshi wawili wa Kenya. Viongozi wa Kenya wamethibitisha kutekwa nyara wanajeshi hao. Kabla ya hapo siku ya Jumamosi, wanamgambo wa al Shabab walishambulia kituo cha polisi kilichoko katika mji wa Liboi kwenye eneo la mpaka wa Kenya na Somalia na kusababisha watu sita kuuawa wakiwemo polisi wawili. Wakati huohuo, Rais wa Somalia amesema kuwa, kundi la al Shabab bado ni tishio katika eneo na ulimwenguni mzima. Rais Hassan Sheikh Mahmoud ameongeza kuwa, ijapokuwa kundi hilo limepoteza udhibiti wa maeneo mengi nchini humo, amma bado linaendeleza operesheni katika maeneo mbalimbali

JESHI LA SYRIA LAZIDI KUWARUDISHA NYUMA WAASI

Pamoja na kuongezeka njama mbalimbali  za madola ya Magharibi kwa kushirikiana na baadhi ya nchi za eneo, dhidi ya Syria, jeshi la nchi hiyo limezidi kupiga hatua kubwa katika mapambano yake na waasi. Katika oparesheni za hapo jana katika maeneo tofauti ya nchi hiyo, waasi wanaoungwa mkono na Magharibi, utawala haramu wa Kizayuni na vibaraka wao wa eneo, walipata kipigo kikali kutoka kwa jeshi la Syria na wengi wao kuangamizwa.
Aidha jeshi hilo limefanikiwa kudhibiti asilimia 80 ya mji wote wa Al-Qusair kusini mwa nchi hiyo. Mbali na hayo, karibu waasi 50 waliokuwa wakipambana dhidi ya serikali halali ya Damascus katika maeneo tofauti ya nchi hiyo, ikiwemo Damascus, Idlib na Homs, wamejisalimisha kwa vikosi vya serikali. Suala hilo limezusha hofu kubwa katika safu za waasi na hivyo kuomba uungaji mkono zaidi wa kijeshi na kifedha kutoka kwa baadhi ya nchi za Kiarabu na za Magharibi.

Sunday, May 26, 2013

GAZETI LA ANNUUR MAY 25, 2013

ANNUUR 1072 by MZALENDO.NET

JESHI LA UFARANSA LAANZA KUONDOA ZANA ZAKE MALI

Msafara wa malori makubwa umeondoka katika kambi ya Wafaransa karibu na mji mkuu, Bamako, kuelekea kusini katika nchi ya jirani, Ivory Coast. Ufaransa ilituma wanajeshi 4,500 nchini Mali mwezi wa Januari kwenda kupambana na wapiganaji wa Kiislamu. Inapanga kukabidhi jukumu hilo kwa jeshi la Mali na kikosi cha Umoja wa Mataifa mwezi Julai.
Wanajeshi wa Ufaransa walipoingia Mali walishangiliwa sana. Wananchi wengi wa Mali wanaogopa wanajeshi hao kuondoka. Msafara ulioondoka Bamako ni mkubwa, lakini Wafaransa wanasisitiza kuwa kwa sasa wanaondosha zana na malori ambayo hayahitajiki. Kwa sasa vifaru na magari makubwa ya deraya yatabaki kaskazini mwa Mali. Ufaransa bado ina wanajeshi 3,800 katika koloni yake hiyo ya zamani.
Inasema itapunguza idadi hadi 2,000 mwezi Septemba, na watabaki 1,000 tu ufikapo mwisho wa mwaka.
Shughuli za kuhama zimeanza siku mbili tu baada ya wapiganaji wa Kiislamu kulenga mgodi wa uranium katika nchi jirani na Mali, yaani Niger. Haijulikani shambulio litaathiri vipi matumizi ya jeshi la Ufaransa katika kanda hiyo ya Afrika Magharibi.

BANDARI YA DAR ES SALAAM KICHOCHEO KIKUBWA CHA UCHUMI- WB

Tanzania na mataifa jirani ya Afrika Mashariki yanatajwa kuwa yanaweza kuboresha pato la ndani la mwaka – GDP – kama yatachukua hatua za kuboresha ubora wa bandari ya Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa ripoti mpya iliyopewa kichwa cha ‘Opening the Gates: How the port of Dar es Salaam can transform Tanzania’ iliyoandikwa na Jacques Morisset, mchumi mkuu wa Benki ya Dunia kwa Tanzania, Uganda na Burundi, Tanzania na majirani zake wanaweza kuongeza pato lao la ndani kwa kiwango kikubwa. Ripoti hiyo inasema Tanzania inaweza kuongeza pato lake la ndani kwa kiasi cha dola bilioni 1.8  na nchi jirani zinaweza kupandisha pato la ndani kwa dola milioni 830 kwa mwaka, kiwango ambacho kinaelezewa ni hasara iliyotokea mwaka 2012.
Ripoti hiyo inasema kuwa bandari ya Dar es Salaam iko katika njia kuu ya biashara ya Tanzania kwa asilimia 90, na inashughulikia bidhaa zinazogharimu dola bilioni 15 kwa mwaka, sawa na asilimia 60 ya pato la ndani la Tanzania kwa mwaka 2012. Bandari hiyo pia inaelezewa kuwa inatumiwa na majirani sita wa Tanzania, ambao nchi zao hazina bandari, nchi hizo ni Malawi, Zambia, Burundi, Rwanda, Uganda na mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Mwaka 2012 pekee, ripoti inasema hasara ya jumla inayoelezewa ambayo imetokea katika bandari hiyo imefikia dola bilioni 1.8 kwa uchumi wa Tanzania na dola milioni 830 kwa nchi jirani. Hasara ambayo ni sawa na asilimia saba ya pato la ndani la mwaka la Tanzania, na kwa kiasi kikubwa imeathiri wanunuzi wa ndani, biashara na mashirika ya serikali.
Moja ya sababu ambazo inaelezewa zimechangia katika hasara hii ni utendaji mbaya wa bandari ya Dar es Salaam ambao umezigharimu nchi nyingine jirani nazo kupata hasara, na hivyo kulazimika kulipa fedha zaidi kwa bidhaa zinazoagiwa kutoka nje, ikiwemo bidhaa za msingi kama vile mafuta ghafi, simenti, mbolea na madawa. Moja ya vigezo  vilivyoelezewa katika ripoti ambavyo vinachangia katika kusababisha  hasara ni pamoja na uchelewesho unaozikabili meli ambazo zinafika katika bandari ya Dar es Salaam.  Katikati ya mwaka 2012, meli zilisubiri kwa takriban siku 10 ili kuweza kuruhusiwa kutia nagan na siku 10 nyingine za ziada ili kuweza kushusha mizigo.  Rushwa pia imetajwa kuwa ni kigezo kingine kinachochangia katika utendaji mbaya wa Bandar, kama chanzo cha utendaji mbaya na kusababisha hasara kubwa.

MWANAJESHI APIGWA KISU PARIS

Mwanajeshi mmoja wa Ufaransa amedungwa kisu shingoni na mtu asiyejulikana alipokuwa akishika doria mjini Paris.Rais wa Ufaransa Francois Hollande amesema kwa hivi sasa shambulio hilo haliwezi kuhusishwa na mauaji ya mwanajeshi mjini London Uingereza yaliyotokea mapema wiki hii.Mshambuliaji huyo alitoroka baada ya kumchoma kisu Cedric Cordier mwenye umri wa miaka 23 jana jioni katika mtaa wa La Defence ambao wakati wa wikiendi hujaa watu wenye kufanya manunuzi.Afisi ya mwendesha mashitaka wa mji huo imesema wachunguzi wa kukabiliana na ugaidi watashughulikia uchunguzi wa shambulio hilo ambalo lilinaswa katika kamera.Mwanajeshi huyo aliyekuwa amevaa sare za kijeshi na alikuwa na silaha,alikuwa akishika doria kama mojawapo ya mipango ya Ufaransa ya kukabiliana na visa vya kigaidi katika maeneo muhimu ya kibiashara, usafiri na yanayotembelewa na watalii katikati mwa mji mkuu Paris.Mshambuliaji huyo ambaye  polisi wamesema ni mrefu wa mita 1.9,mwenye ndevu alikuwa amevalia fulana na suruali nyeusi alimfikia mwanajeshi huyo na kumchoma kisu na baadae kutangamana na umati bila kutamka neno lolote.

ROKETI ZAJERUHI WATANO BEIRUT

Watu watano wamejeruhiwa leo wakati makombora mawili ya kurushwa kwa roketi kuripuka katika eneo linalokaliwa na Washia wengi la kusini mwa Beirut nchini Lebanon ambayo ni ngome ya kundi la Hezbollah.Roketi la kwanza lilishambulia kampuni ya kuuza magari ambapo watu wanne walijeruhiwa na magari kuharibiwa.Hii ni mara ya kwanza mji mkuu wa Lebanon Beirut kulengwa katika mzozo wa nchi jirani ya Syria ambako kundi la wanamgambo la Hezbollah linashirikiana na wanajeshi wa utawala wa Rais Bashar al- Assad kukabiliana na waasi wanaotaka kumn'goa rais huyo madarakani.Shambulio hilo la leo linakuja saa chache baada ya kiongozi wa kundi hilo la Hezbollah Hassan Nasrallah kutangaza ushindi nchini Syria.Nasrallah alikuwa akizungumza katika sherehe za kuadhimisha miaka 13 tangu kuondoka kwa majeshi ya Israel nchini Lebanon na kuongeza kuwa amekuwa akiahidi ushindi na sasa anaahidi ushindi mpya nchini Syria.Nasrallah ameapa kumuunga mkono Assad akisisitiza kuwa maslahi yao pia yako hatarini katika vita hivyo vya miaka miwili vya Syria.

BRAZIL KUZISAMEHE MADENI YAKE NCHI ZA AFRIKA

Brazil imetangaza kuwa itazisamehe nchi za Kiafrika madeni ya karibu dola milioni 900 au kuyachunguza upya madeni hayo. Habari hiyo imetangazwa katika safari ya tatu ya Rais Dilma Rousseff wa Brazil barani Afrika ambako safari hii ameshiriki katika mkutano wa Umoja wa Afrika uliofanyika hapo jana mjini Addis Ababa Ethiopia pamoja na maadhimisho ya kuasisiwa AU. Rais Rousseff aidha amesema miongoni mwa stratejia za mambo ya nje za Brazil ni kuimarisha uhusiano maalumu na nchi za Kiafrika na kwamba nchi yake tayari imekwishashughulikia madeni yaliyokuwa yamerundikana tangu miaka ya 70. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Brazil amesema, kuangaliwa tena madeni ya baadhi ya nchi za Afrika kunamaanisha kuzingatiwa viwango bora zaidi vya riba na muda mrefu wa kulipa. Miongoni mwa nchi zitakazofaidika na suala hilo  ni Congo-Brazaville, Tanzania, Zambia, Ivory Coast, Gabon, Guinea, Guinea Bissau, Kongo DRC na Sudan.

UMOJA WA ULAYA WATAKIWA KULINDA ARDHI ZA PALESTINA

Kundi la mashirikia 80 ya kimataifa ya utoaji misaada limeutaka Umoja wa Ulaya EU kutekeleza ahadi zake ilizotoa mwaka uliopita za kulinda ardhi za Palestina dhidi ya mpango wa Israel wa kupanua vitongoji vya walowezi wa Kizayuni. Jumuiya ya Kimataifa ya Taasisi kwa ajili ya Maendeleo (AIDA) imesema kwamba, EU haijachukua hatua za kutosha tangu Mawaziri wa Mambo Nje wa umoja huo walipokosoa siasa za kupanuliwa vitongoji za Israel katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan mwezi Mei na kuahidi kukabiliana nazo. Kwa mujibu wa jumuiya hiyo, tangu mwezi Mei mwaka uliopita Israel imebomoa nyumba 535 za Wapalestina na majengo mengineyo yakiwemo 30 yaliyojengwa kwa msaada wa EU, na kujenga nyumba 600 za walowezi wa Kizayuni. Ripoti hiyo aidha imeongeza kwamba, kutokana na hatua hizo za Israel tangu mwaka uliopita Wapalestina wasiopungua 784 wamekosa makaazi.
Kuendelea ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu ya Palestina, kumekuwa kikwazo kikubwa cha kupatikana amani Mashariki ya Kati na kuundwa nchi huru ya Palestina.

KATIBA YA TUNISIA IMEZINGATIA UISLAM


Kiongozi wa chama Kiislamu cha Enahdha nchini Tunisia Rashid al Ghanoushi amesema katiba mpya ya Tunisia imeandikwa kwa mujibu wa misingi ya Kiislamu. Akizungumza Jumamosi mjini Tunis katika semina iliyokuwa na anwani ya 'Kutekeleza Uislamu katika Siasa', Ghanushi alisema Baraza la Waasisi Tunisia lilitumia misingi ya Kiislamu kuandika katiba mpya ya nchi hiyo. Ghanushi ambaye ni mkuu wa chama cha Enahdha kinachoongoza muungano tawala nchini humo amesema katiba mpya imetegemea Uislamu kwa kuzingatia hali inayotawala ulimwengu wa sasa.
Mwezi ujao wa Juni Baraza la Waasisi Tunisia linatazamiwa kuchunguza rasimu ya katiba mpya ili hatimaye katiba hiyo iidhinishwe na wananchi katika kura ya maoni.
Tunisia ni kati ya nchi ambazo zimeshuhudia mwamko wa Kiislamu ambapo mtawala kibaraka wa nchi hiyo dikteta Zainul Abidin Bin Ali alitimuliwa madarakani 2011.

MUSEVEN ASEMA ICC INA NJAMA ZA KUMKAMATA KENYATTA


Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesema kuna njama ya kumtia mbaroni Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya huko The Hague wakati kesi yake itakapoanza katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC Julai 9.
Museveni ameyadokeza hayo mjini Addis Ababa Ethiopia wakati akizungumza na viongozi wa Jumuiya ya IGAD ya Pembe na Mashariki mwa Afrika.
Katika hotuba yake ya Ijumaa usiku, Museveni alisema ICC haina nia njema katika kesi inayowahusu Wakenya watatu ambao ni rais Kenyatta, naibu wake William Ruto na mwandishi habari Joshua Sang.
Museveni amenukuliwa akisema kuwa viongozi wa IGAD hawataafiki Kenyatta kuhudhuria kesi ya ICC iwapo nia ni kumtia mbaroni. Ameonya kuwa iwapo ICC haitaweka wazi nia yake, basi uhusiano wa ICC na Afrika utazorota. Amesema mahakama hiyo ya kimataifa inapaswa kuwaheshimu viongozi wa Afrika. Rais Museveni anaongoza mkakati wa viongozi wa Umoja wa Afrika wanaotaka ICC itupilie mbali kesi dhidi ya Kenyatta. Imearifiwa kuwa nchi zote za Afrika isipokuwa Botswana zimeunga mkono mtazamo wa Museveni. Hali kadhalika mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Bi. Nkosazana Dlamini Zuma amenukuliwa akisema matatizo ya Afrika yanapaswa kutatuliwa na Waafrika wenyewe.

Saturday, May 25, 2013

WAISLAM WA MYANMAR WAWEKEWA KIKOMO CHA KUZAA


Wakuu wa jimbo la Magharibi nchini Myanmar wamepitisha sheria inayopiga marufuku familia za Waislamu wa kabila la Rohingya kuzaa watoto zaidi ya wawili. Kwa kutumia kisingizio cha kupunguza mivutano kati ya Waislamu na Mabudha ambayo imesababisha machafuko na mashambulio makubwa na ya kikatili dhidi ya jamii ya wachache ya Waislamu wa Myanmar, wakuu wa jimbo la Rakhin wamepitisha sheria inayowataka Waislamu wasiwe na watoto zaidi ya wawili. Duru za habari zimemnukuu afisa mmoja wa jimbo hilo akisema kuwa sheria hiyo itahusisha miji miwili iliyoko kwenye mpaka wa pamoja wa Myanmar na Bangladesh na ambayo ndiyo yenye idadi kubwa zaidi ya Waislamu. Wein Maying, msemaji wa serikali ya jimbo la Rakhin ametangaza kuwa sheria hiyo ilipitishwa wiki mbili zilizopita baada ya tume iliyoundwa na serikali kupendekeza ianzishwe sera ya uzazi wa mpangilio ili kupunguza mivutano katika eneo hilo lenye mgogoro.
Mashambulio na vitendo vya kikatili dhidi ya Waislamu nchini Myanmar vilianza tangu mwaka mmoja nyuma ambapo Mabudha wenye silaha baridi wamezishambulia nyumba za Waislamu na kuwaua kwa halaiki mamia miongoni mwao na kuwafanya wengine zaidi ya laki moja kuwa wakimbizi baada ya kubaki bila makaazi. Serikali ya Myanmar haiwatambui Waislamu wa kabila la Rohingya kuwa ni raia wa nchi hiyo bali inadai kwamba ni wahajiri wa Kibangladeshi. Hii ni katika hali ambayo kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa Waislamu wa kabila la Rohingya ni moja ya jamii za wachache duniani wanaonyongeshwa na kukabiliwa na manyanyaso na mateso makubwa

ISRAEL YAPANGA SHERIA YA KUMPIGA RISASI KILA MPALESTINA MWENYE JIWE

Majenerali wa Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel wameliomba baraza la mawaziri la utawala huo haramu litoe kibali cha kushadidisha ukandamizaji dhidi ya Wapalestina wa Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan. Gazeti la Kizayuni la Maariv limeandika kuwa majenerali wa jeshi la Israel wanasisitiza kuwa kuna ulazima wa kuchukua hatua kali zaidi za ukandamizaji ili kukomesha machafuko katika eneo la Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan. Maariv limemnukuu Jenerali Danny Yatom akisema kuwa baraza la mawaziri linapaswa kutoa kibali haraka kwa jeshi ili lichukue hatua kali zaidi za ukandamizaji dhidi ya Wapalestina na kuzuia kuenea machafuko na kuanza Intifadha ya Tatu. Yatom, ambaye ni mkuu wa zamani wa Shirika la Ujasusi la Israel Mossad amesema jeshi la Israel haliwezi kubaki kuwa mtazamaji tu  wa machafuko katika Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan bali linapaswa kutoa radiamali na kuwaua wapinzani. Jenerali huyo wa zamani wa jeshi la utawala haramu wa Israel amesisitiza juu ya ulazima wa kuwaua Wapalestina wa umri wowote ule na kubainisha kwamba bila ya kuhofu chochote vikosi vya jeshi la Israel vichukue hatua ya kumfyatulia risasi Mpalestina wa umri wowote ule atakayekuwa na jiwe mkononi mwake

MACHAFUKO YAENEA NJE YA MJI MKUU WA SWEDEN


Machafuko yameenea nje ya mji mkuu wa Sweden Stockholm, ambako waandamanaji wamechoma moto magari na nyumba katika miji miwili ya nchi hiyo. Polisi imesema kuwa, waandamanaji wamechoma moto shule, majumba na magari kadhaa katika miji ya Oerebto na Sodertalje nje ya mji wa Stockholm. Wakati huo huo magari yameendelea kuchomwa katika vitongoji kadhaa vya wahamiaji kwa usiku wa 6 mtawalia wa machafuko yaliyoukumba mji mkuu wa Sweden, suala lililoilazimu polisi ya mji huo kuomba msaada.
Maandamano yalianza nchini Sweden May 19, siku 6 baada ya polisi kumpiga risasi na kumuua mwanaume wa miaka 69 nyumbani kwake kwenye eneo la wakaazi wengi masikini la Husby. Kitendo hicho kimeamsha hasira ya vijana wa eneo hilo wanaodai kwamba serikali inawabagua.

JESHI LA NIGERIA LAHARIBU KAMBI YA BOKO HARAM


Jeshi la Nigeria limetangaza kuwa, limeharibu na kudhibiti kambi kadhaa muhimu zilizokuwa zikitumiwa na kundi la Boko Haram kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Brigadia Christ Olukolade afisa wa habari wa jeshi hilo amesema, kambi hizo zilikuwa zikitumiwa katika kupanga operseheni za waasi na walikuwa wakishambulia maeneo ya karibu kutokea huko.
Wiki iliyopita askari 2,000 walipelekwa kwenye eneo hilo katika operesheni kubwa ya kupambana na kundi la Boko Haram.  Hatua hiyo ilichukuliwa baada ya Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria kutangaza hali ya hatari katika majimbo matatu ya kaskazini mashariki mwa nchi yanayohesabiwa kuwa ngome kuu ya kundi hilo. Wakati huo huo wanawake na watoto 6 waliokuwa wametekwa nyara na wanamgambo wa Boko Haram wameachiliwa huru.

NIGER WAMKOMBOA MWANAJESHI MIKONONI MWA WAASI

Karidjo Mahamadou Waziri wa Ulinzi wa Niger amesema kuwa, vikosi vya jeshi la nchi hiyo vikishirikiana na vya Ufaransa vimefanya oparesheni kubwa katika mji wa Agadez na kufanikiwa kumuokoa mwanajeshi wa nchi hiyo aliyekuwa akishikiliwa mateka na waasi. Karidjo Mahamadou amesema kuwa, kwenye oparesheni hiyo wateka nyara wawili waliuawa wakati wa kufyatuliana risasi na wanajeshi wa Niger wakishirikiana na wa Ufaransa. Hii ni katika hali ambayo, kabla ya hapo, Waziri wa Ulinzi wa Niger alikuwa amekadhibisha taarifa za kutekwa nyara mwanajeshi wa Niger na kundi la watu wanaobeba silaha nchini humo. Mara baada ya kutokea shambulio la waasi huko kaskazini mwa Niger, Rais Francois Hollande wa Ufaransa alitangaza kuendelea kubaki majeshi ya nchi hiyo barani Afrika kwa kisingizio cha kupambana na makundi ya kigaidi na kuzisaidia nchi za Kiafrika.

ISRAEL YAONGEZA MISAADA KWA WAASI WA SYRIA

Mamia ya majeruhi ya wanamgambo wa makundi ya waasi nchini Syria wamehamishiwa kwenye hospitali za utawala wa Kizayuni wa Israel kwa minajili ya kupatiwa matibabu. Gazeti la al Manar la Palestina limeandika kuwa, kiwango cha misaada ya utawala wa Kizayuni wa Israel kwa makundi ya waasi ya Syria ni kikubwa, na kueleza kwamba utawala wa Israel unadhamini mahitajio ya kivita ya magaidi na kuwapatia huduma nyingine nyingi kwa lengo la kuongeza mashambulizi yao dhidi ya serikali ya Damascus. Gazeti la al Manar limefichua kwamba, yapata miezi saba iliyopita, utawala wa Israel ilianza  kujenga hospitali ya kijeshi katika moja ya kambi zake zilizoko katika eneo la milima ya Golan ya Syria inayokaliwa kwa mabavu na utawala wa Israel kwa minajili ya kutoa huduma za kimatibabu kwa waasi wa Syria. Hii ni katika hali ambayo, Saudi Arabia  na Qatar zimeupatia utawala wa Israel mamia ya milioni ya dola kutokana na huduma inazozitoa kwa makundi ya waasi ya Syria.

WAISLAM WAINGIWA NA HOFU YA UKANDAMIZAJI NCHINI UINGEREZA

Kusambazwa hivi karibuni picha zilizoonyesha kuuawa kinyama kwa askari mmoja wa Uingereza katika moja ya mitaa ya London kumeongeza wasiwasi wa Waislamu wa nchi hiyo walio na hofu ya kuongezeka vitendo vya dhulma na ukandamizaji dhidi yao. Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Kiislamu ya Uingereza imetoa taarifa ikikosoa kuenezwa propaganda dhidi ya Uislamu kufuatia mauaji hayo na kutaka kusimamishwa mara moja kwa uchochezi wa chuki unaofanywa dhidi ya Waislamu wa nchi hiyo. Kamisheni hiyo imesisitiza kwamba polisi ya nchi hiyo inapasa kuchukua hatua za dharura za kulinda usalama wa Waislamu pamoja na kukabiliana na makundi ya ubaguzi wa rangi yanayotaka kutumia vibaya tukio hilo dhidi ya Waislamu. Kamisheni hiyo pia imeitaka polisi ya London kuimarisha usalama katika misikiti, shule na vituo vya Kiislamu mjini humo. Kuakisiwa kwa kiwango kikubwa kwa mauaji ya askari huyo wa Uingereza na vyombo vya habari vya nchi hiyo na wakati huohuo kuhusishwa mauaji hayo na Waislamu kumepelekea baadhi ya makundi yenye fikra na mielekeo ya kupindukia mipaka kuwatisha Waislamu na kuonya kwamba yatalipiza kisasi dhidi yao. Askari huyo mwenye umri wa miaka 25 kwa jina la Lee Rigby aliuawa kwa kisu siku ya Jumatano katika mtaa wa Woolwich kusini mashariki mwa London. Mara tu baada ya kuawa askari huyo vyombo vya habari vya Uingereza viliwaarifisha wahusika wa tukio hilo kuwa ni vijana wawili wa Kiislamu na kisha kurusha hewani ripoti nyingi hasi dhidi ya Waislamu. Kuafutaia mauji hayo, David Cameron Waziri Mkuu wa Uingereza ambaye alikuwa safarini nchini Ufaransa alikatiza safari hiyo na kurejea Uingereza kwa lengo la kuongoza kikao cha dharura cha kuchunguza tukio hilo. Akizungumza baada ya kumalizika kikao hicho alisema kuwa lawama za mauaji hayo zinapaswa kuelekezwa kwa waliohusika tu bila ya kuihusisha dini yoyote. Cameron amesisitiza kwamba wananchi wote wa Uingereza bila kujali dini wala utamaduni wao wamekasirishwa na kulaani tukio hilo la kinyama na kuongeza kuwa tukio hilo si tu kwamba limeshambulia Uingereza na  mfumo wa maisha wa raia wa nchi hiyo bali pia ni hiana ya wazi dhidi ya Uislamu na Waislamu wanaoishi nchini humo. Amesisitiza kwamba hakuna sehemu yoyote katika Uislamu ambapo kitendo kama hicho kinahalalishwa. Taasisi na mashirika tofauti ya Kiislamu nchini Uingereza likiwemo Baraza la Waislamu wa nchi hiyo yametoa taarifa tofauti yakilaani tukio hilo na kusisitiza kuwa Uislamu hauungi mkono kitendo kama hicho cha kishetani. Taasisi hizo zimetaka hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi ya wahalifu waliohusika na mauaji hayo kwa madai eti ya kuwatetea Waislamu. Wakati huohuo kundi moja la wabaguzi wa rangi linalodai kutetea maslahi ya Waingereza siku ya Jumatano lilikusanyika katika eneo la tukio hilo na kupiga nara za chuki na ubaguzi wa rangi dhidi ya Waislamu. Tunakumbusha hapa kuwa vitendo vya chuki na uadui vimeongezeka sana dhidi ya Waislamu wanaoishi katika nchi za Ulaya katika miaka ya hivi karibuni.

Friday, May 24, 2013

AU YASHEREHEKEA MIAKA 50


Wageni mashuhuri na marais wa Afrika wameanza kuwasili mjini Addis Ababa Ethiopia kwa sherehe za kuadhimisha miaka hamsini tangu kuanzishwa kwa Muungano wa Afrika. Muungano wa Afrika wakati huo ukijulikana kama OAU,uligeuza jina na kujulikana kama AU mnamo mwaka.  Hapo kesho Jumamosi kutakuwa na sherehe za kilele kuadhimisha miaka hamsini ya AU na Zitahudhuriwa na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na marais wengine wa Afrika. Kauli mbiu ya sherehe za hapo kesho ni mjadala mkuu kuhusu ushirikiano wa nchi za Afrika na kuimarishwa kwa muungano huo.
Mwenyekiti wa tume ya muungano huo, Dr Nkosazana Dlamini Zuma, anaseme kuwa hii itakuwa fursa kwa AU kujadili kuhusu uwezo wa bara hili na ambacho kinaweza kufikiwa katika miaka hamsini ijayo. Sherehe za AU zinakuja wakati swali kuu kwa AU ni kesi zinazowakabili washukiwa wakuu wa ghasia za baada ya uchaguzi wa Kenya mwaka 2007/08 Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto pamoja na mtangazaji wa redio Joshua Arap inaendelea katika mahakama ya kimataifa ya ICC. Duru zinasema kuwa huenda mawaziri wa mambo ya kigeni wa nchi za Afrika wamekubaliana kuhusu azimio linalotaka kesi ya washukiwa hao kurejeshwa Kenya ambako inaweza kusikilizwa na hatua kuchukuliwa dhidi ya watakaopatwa na makosa.
Shereha hizi pia zinakuja wakati bara la Afrika linashuhudia migogoro nchini Mali, DRCongo huku Misri ikiwa bado haijatengamaa baada ya kufanyika mapinduzi ya kiraia yaliyomng'oa mamlakani aliyekuwa rais Hosni Mubarak. Lakini mwenyekiti wa AU ana matumaini kuwa Afrika iko kwenye mkondo mzuri wa kimaendeleo. Katika hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 21 wa AU, Dlamini Zuma alisema kuwa Afrika imekuwa kiuchumi katika muongo mmoja uliopita, imeshuhudia maendeleo ya kiuchumi , ustawi wa kikanda , uimarishwaji wa miundo mbinu na ushirikiano wa kikanda. Sherehe hizi ambazo zitafuatwa na mkutano wa siku mbili wa marais wa AU, zitatoa fursa kwa wananchi wa bara la Afrika kuangazia ufanisi wa Muungano huo.

TALIBAN WASHAMBULIA KABUL


Miripuko na milio ya risasi imesikika katikati ya Kabul leo hii wakati kundi la Taliban liliposhambulia karibu na kituo cha ujasusi na makao makuu ya kikosi cha serikali chenye kulinda makampuni ya kigeni.
Mashambulizi hayo yamekuja wiki moja baada mashambulizi mengine ya  kujitowa muhanga kwa kutumia gari lililotegwa bomu kuuwa watu 15 wakiwemo Wamarekani watano ikiwa ni shambulio baya kabisa kuwahi kushuhudiwa katika mji mkuu huo wa Afghanistan kwa takriban mwaka mmoja. Takriban mirupuko miwili ilipiga katikati ya Kabul saa nane mchana leo hii na milio ya risasi ilisikika baada ya vikosi vya usalama kukimbilia katika eneo hilo. Inaelezwa watu wenye silaha wamelikalia jengo moja na kwamba vikosi vya usalama vilikuwa vikiendelea kupambana nao.

LAGARDE ATINGA TENA MAHAKAMANO


Mahakama moja nchini Ufaransa inamuhoji kwa siku ya pili mfululizo Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF, Christine Lagarde, juu ya dhima yake katika kuagiza malipo ya mfanyabiashara mmoja hapo mwaka 2008 wakati akiwa waziri wa fedha wa Ufaransa. Lagarde aliandaa makubaliano ambayo yalipelekea kulipwa kwa fidia ya zaidi ya euro milioni 285 kwa Bernard Tapie. Fedha hizo zikijumuishwa na riba kwa jumla zinafikia euro milioni 400.Baada ya kusailiwa kwa masaa 12 hapo jana, mkuu huyo wa IMF amesema kikao hicho cha mahakama kingeliendelea leo hii. Mahakama hiyo haikutowa taarifa yoyote ile rasmi. Tapie ambaye alikuwa mmliki mkuu wa kampuni ya Adidas alidai kwamba alidhulumiwa na Benki ya Lyonnais inayomilikiwa na serikali wakati ilipoandaa mipango ya kuuzwa kwa kampuni hiyo ya vifaa vya michezo hapo mwaka 1992. Waendesha mashtaka wanamshuku Lagarde kuzifanyia ubadhirifu fedha za umma kwa sababu fedha zilizotumika kusuluhisha mzozo huo zilitoka katika hazina ya taifa.

KUNDI LA MUJAO LATISHIA KUISHAMBULIA UFARANSA POPOTE DUNIANI


Baada ya Kundi la kigaidi linaloongozwa na raia wa Algeria Mokhtar Belmokhtar kumedai kutekeleza mashambulizi mawili ya kujitoa muhanga na kuua watu ishirini limetishia kutekeleza mashambulizi zaidi nchini humo na nchi nyingine itakayoinuka kinyume na kundi hilo. Kiongozi huyo amekiri kuendeleza mashambulizi zaidi taarifa ambayo imepatikana kupitia mtandao wa kundi hilo la kigaidi na kutishia taifa la Ufaransa na taifa lingine lolote litakalothubutu kuingilia vita vya waislamu hao wenye msimamo mkali nchini Mali. Watu zaidi ya ishirini wanakadiriwa kuuawa kwenye shambulio la bomu la kujitoa muhanga nchini Niger kwenye machimbo ya Uranium yanayomilikiwa na kampuni ya Ufaransa, shambulio la ulipizaji kisasi kufuatia majeshi ya Ufaransa kuvamia kaskazini mwa Mali.
Msemaji wa kundi la MUJAO la nchini Niger, Abu Walid Sahraoui amekiri kundi lake kuhusika na shambulio hilo na kuongeza kuwa litaendelea kushambulia maslahi ya taifa la Ufaransa popote duniani. Oumaru Garba ni mkuu wa operesheni ya kijeshi kwenye eneo la Arlit ambako shambulio hilo limetekelezwa, amesema kuwa juhudi za makundi ya wapiganaji wa kiislamu kuharibu usalama hazitafua dafu. Wanaharakati nchini humo wanalaani shambulio hilo na kuitaka serikali kuzidisha usalama kwenye maeneo ya mpakani na nchi ya mali kwakuwa wapiganaji hao ndiko wanakojipenyeza kutekeleza mashambulio hayo. Kundi la MUJAO limefurushwa kaskazini mwa Mali baada ya kushikilia maeneo hayo kwa miezi kadhaa kabla ya uvamizi wa majeshi ya Ufaransa na vile vikosi vya Mali.

MAJESHI YA SYRIA YAMTIA MBARONI KAMANDA WA KUNDI LA AN NUSRA


Wanajeshi wa Syria wameua makumi ya waasi katika mapambano ya kuuokomboa mji wa kiistratijia wa Qusayr na katika maeneo tofauti ya mikoa ya Halab, Damascus na Homs.
Vikosi vya Syria aidha vimesema kuwa vimefanikiwa kumtia mbaroni kamanda wa genge la Jabhat an Nusra huko Qusayr na kuvunja jaribio la waasi hao la kuripua magari yaliyokuwa yametegwa mabomu huko Rif Dimashq na ambayo yalikuwa na karibu kilo 1300 za miripuko.
Mwandishi wa televisheni ya al Alam ameripoti kuwa jeshi la Syria limefanikiwa kuteketeza shehena kubwa ya silaha na miripuko katika eneo la kaskazini mwa mkoa wa Qusayr na kuua makumi ya waasi.
Vile vile jeshi la Syria limesema kuwa limefanikiwa kuua waasi zaidi ya 20 katika viunga vya Halab, kukamata silaha nyingi na kuteketeza makumi ya magari ya kivita ya waasi hao.

WAPALESTINA WAANDAMANA KUPINGA SAFARI YA KERRY

Add caption

Mamia ya wananchi wa Palestina wameandamana kupinga safari ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni. Taarifa zinasema kuwa, Wapalestina hao wamefanya maandamano hayo katika Ukingo wa Magharibi mwa Mto Jordan sambamba na kuwazili John Kerry katika katika ukingo huo huku akipiga nara za kulaani siasa za Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati na kuitaka Washington iache kuunga mkono utawala wa Kizayuni wa Israel unaotenda jinai za kila namna dhidi ya Wapalestina.
Waaandamanaji hao pia wamewataka wakuu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina kuacha kufanya mazungumzo na Wazayuni kwa sababu hayana faida zozote kwa taifa la Palestina.

WAASI WA MALI WADAI KUWA WALISHAMBULIA NIGER

Kundi moja la waasi wa Mali linalojulikana kwa jina la Harakati ya Tawhid na Jihadi ya Afrika Magharibi (MUJAO) limedai kuwa ndilo lililohusika na miripuko miliwi ya magari yaliyokuwa yametegwa mabomu katika nchi jirani ya Niger na kupelekea zaidi ya watu 20 kuuawa. Msemaji wa kundi hilo, Abu Walid Sahraoui amesema kuwa, kundi hilo lilifanya shambulizi hilo jana Alkhamisi ili kuliadhibu njeshi la Niger kwa kushirikiana na mkoloni wa Ulaya, Ufaransa kuvamia na kufanya mauaji nchini Mali. Miripuko hiyo imetokea kwenye kambi moja ya jeshi na katika mgodi mmoja wa urani katika miji ya Agadez na Artil huko kaskazini magharibi mwa Niger na kupelekea watu wasiopungua 26 kuuawa 20 kati yao wakiwa ni wanajeshi. Mashambulizi ya namna hiyo ni ya kwanza kutokea nchini Niger tangu nchi hiyo ilipoamua kushirikiana na Ufansa katika vita dhidi ya waasi nchini Mali. Ufaransa ambayo ni mkoloni mkongwe wa Ulaya huko magharibi mwa Afrika, iliivamia Mali tarehe 11 Januari mwaka huu kwa madai ya kupambana na waasi, uvamizi ambao umesababisha mgogoro mkubwa wa kibinaadamu katika maeneo ya kaskazini mwa Mali huku maafisa wa kijeshi wa Mali wakiilaumu Ufaransa kuwa ilikuwa na nia ya kujizatiti kijeshi tu katika eneo hilo na si kumaliza uasi. Hadi leo Ufaransa imekataa kuondoka kwenye eneo hilo lenye utajiri mkubwa wa maliasili kwa madai kuwa waasi bado wana ushawishi kwenye maeneo hayo.

KATIBU MKUU WA UN AENDELEA NA SAFARI ZAKE AFRIKA

Ban Ki moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameendelea na safari yake ya kuzitembelea nchi za eneo la Maziwa Makubwa la katikati mwa Afrika iliyoanzia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Jana Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa aliwasili katika mji wenye mgogoro wa kivita wa Goma wa mashariki mwa Kongo DRC kwa lengo la kuizindua jamii ya kimataifa kuhusu nchi hiyo iliyokumbwa na vita vya ndani kwa miaka mingi sasa huku mamilioni ya watu wakiendelea kuteseka kutokana na mgogoro huo. Ban Ki moon aliwasili mjini humo masaa machache baada ya waasi wa M23 kutangaza kusimamisha vita karibu na mji huo ili kuruhusu kufanyika kwa usalama safari ya Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa. Safari fupi ya Ban katika mji huo wenye utajiri mkubwa wa madini imefanyika siku tatu tu tangu mapigano makali yazuke kwenye eneo hilo kati ya wanajeshi wa serikali na waasi. Watu wasiopungua 20 wameripotiwa kuuawa katika mapigano hayo mapya yaliyoanza siku ya Jumatatu huku makombora yakiripotiwa kuanguka karibu na mji huo. Mbali na Kongo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametembelea pia nchi jirani na Kongo yaani Rwanda na anatarajiwa kutembelea pia Uganda.

AU YATAKA KESI YA VIONGOZI WA KENYA IFUTWE


Nchi za Afrika zimeunga mkono ombi la Kenya la kutaka kesi ya jinai dhidi ya rais wake kufutwa katika mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC. Duru za kidiplomasia zinasema Umoja wa Afrika umeafiki ombi la Kenya la kutaka kesi dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto iondolewe ICC na badala yake kusikilizwa nchini Kenya. Pendekezo hilo la Kenya lilijadiliwa katika kikao cha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Afrika waliokutana Alkhamisi huko Addis Ababa Ethiopia. Pendekezo hilo linatazamiwa kuidhinishwa katika mkutano wa kilele wa viongozi wa AU ambao watakutana kesho katika mji mkuu huo wa Ethiopia. Serikali ya Kenya imesema kesi za ICC dhidi ya viongozi wake zitahatarisha usalama wa nchi hiyo yenye uchumi mkubwa zaidi mashariki mwa Afrika.
Wakati huo huo Nafie Ali Nafie Mshauri wa Rais Omar el Bashir wa Sudan amesema huenda nchi za Afrika kwa pamoja zikapitisha azimio la kujiondoa ICC. Ikumbukwe ICC imetoa waranti wa kutiwa mbaroni Rais Bashir wa Sudan. Kwingineko Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amesema nchi yake inapinga kesi ya ICC dhidi ya Rais Uhuru Kenytta. Ameyasema hayo baada ya kukutana na Kenyatta mjini Juba siku ya Alkhamisi. ICC inalaumiwa kuwa ina muelekeo wa kisiasa katika kesi zake ambazo zote zinalenga nchi za Afrika.

NI HARAM KUPIGANA DHIDI YA SERIKALI YA SYRIA

Khatibu wa Masjidul az Zaytuniyyah nchini Tunisia amesema kuwa, kile kinachojiri nchini Syria kwa muda wa zaidi ya miaka miwili sasa, ni njama za kutaka kuigawa nchi hiyo. Sheikh Hussein al Obeidi amesisitiza kuwa, Uislamu umeharamisha kupigana dhidi ya Waislamu. Amesema kuwa, jihadi ya uhakika ni kupambana na utawala wa Kizayuni wa Israel, utawala unaowakandamiza wananchi wa Palestina pamoja na kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu huko Quds Tukufu. Sheikh al Obeidi amebainisha kuwa, haijuzu kisheria kwa Waislamu kupambana na nchi ya Kiislamu na kwamba mtu yeyote anayekwenda kupambana na wananchi wa Syria, anatenda jambo la haramu. Khatibu wa Masjidul Zaytuniyyah ameongeza kuwa, Uislamu unapinga kabisa vitendo vya kigaidi na kwamba jambo hilo liko wazi na wala halina shaka yoyote. Mwanachuoni huyo wa Tunisia amewatahadharisha vijana wa nchi hiyo wanaoelekea nchini Syria kwa shabaha ya kupambana na serikali ya Damascus na kusema kuwa, vijana hao wamekuwa wahanga wa 'kusafishwa bongo' zao.

OBAMA, BUSH NA BLAIR WAHUKUMIWE ICC

Noam Chomsky msomi mtajika nchini Marekani amesema kuwa, Rais Barack Obama wa nchi hiyo na kiongozi aliyemtangulia George W. Bush pamoja na Tony Blair Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza wanapaswa kufikishwa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC iliyoko Uholanzi, kujibu tuhuma za kutenda jinai za kivita na kibinadamu nchini Iraq kuanzia mwaka 2003. Mwandishi huyo wa Kimarekani ameongeza kuwa, Obama anahusika na jinai za kuwauwa wananchi wasio na hatia wa Pakistan, Afghanistan, Yemen na Somalia kwa kutoa ruhusa ya kutumiwa ndege zisizo na rubani dhidi ya nchi hizo, kwa kisingizio cha kupambana na makundi ya kigaidi. Matamshi ya Chomsky yanatolewa katika hali ambayo, Rais Obama hapo jana alisikika akisema kwamba, utumiwaji wa ndege hizo zisizo na rubani ni wa kisheria, kiuadilifu na wenye kuleta athari chanya kwa serikali ya Washington.