Duru za habari kutoka Libya zimeripoti kuwa, afisa wa ngazi za juu wa polisi ameuawa na magaidi nchini humo. Luteni Kanali Nasser al-Maghrabi aliyekuwa afisa mwandamizi wa polisi katika eneo la mashariki mwa mji wa Bengazi aliuawa jana na watu wasiojulikana wenye silaha nchini humo. Wakuu wa usalama nchini Libya wamesema mwili wa marehemu ulikutwa karibu na nyumba aliyokuwa akiishi katika mji huo wa Bengazi. Siku ya Alkhamis iliyopita, Mkuu wa Idara ya upelelezi wa jinai katika mji huo, aliuawa na watu wasiojulikana alipokuwa akielekea ofisini kwake. Mji wa Bengazi ulikuwa kitovu cha vuguvugu la mapinduzi dhidi ya utawala wa Muammar Gaddafi dikteta wa zamani wa Libya. Katika siku za hivi karibuni mji huo umegeuka na kuwa uwanja wa vitendo vya mashambulizi dhidi ya viongozi wa serikali ya sasa ya nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO