Kundi la Ansarudeen moja ya makundi ya waasi ya kaskazini mwa Mali linaripotiwa kusonga mbele kuelekea katika moja ya miji muhimu ya nchi hiyo wa Mopti. Habari kutoka Mali zinasema, kundi la Ansarudeen ambalo hivi karibuni lilitangaza kusitisha usimamishaji vita wake wa upande liliokuwa limeutangaza hivi sasa wapiganaji wake wanasonga mbele kuelekea Mopti. Taarifa iliyotolewa na waasi hao imesisitiza kwa mara nyingine tena kwamba, kundi hilo halifungamani tena na ahadi zake ilizotoa katika mazungumzo ya Algeria kwa sababu serikali ya Mali haijachukua hatua zozote za maana za kuhitimisha uhasama na kundi hilo.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, hivi karibuni waasi wa Ansarudeen walikabidhi katiba yao ya kisiasa kwa Rais Blaise Compaore wa Burkina Faso ambaye ni mpatanishi wa mgogoro kati ya serikali ya Mali na waasi wa kaskazini mwa nchi hiyo tokea tarehe Mosi Januari mwaka huu. Katiba hiyo ya kundi la Ansarudeen yenye kurasa 17 imesisitiza juu ya kuwepo serikali ya Kiislamu nchini Mali kwenye katiba yao; kwani zaidi ya asilimia 95 ya wananchi wa nchi hiyo ni Waislamu.

No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO