Waziri Mkuu wa serikali halali iliyochaguliwa na wananchi ya Palestina ametoa wito wa kuitishwa kikao cha Kamati ya Quds ili kukabiliana na mipango ya Wazayuni ya kuuyahudisha mji mtakatifu wa Baytul Muqaddas.
Ismail Hania amesema, mji wa Baytul Muqaddas sio mali ya Wapalestina tu bali ni mali ya Waislamu wote ulimwengu; kwani ndio kibla cha kwanza cha Waislamu. Amesema kuna haja ya kufanyika kikao cha Kamati ya Quds ili kutafuta njia za kukabiliana na mipango na njama za kila leo za utawala wa Kizayuni wa Israel za kutaka kubadilisha muundo wa kijamii na kijiografia wa mji wa Baytul Muqaddas.
Waziri Mkuu wa serikali halali iliyochaguliwa na wananchi ya Palestina amesisitiza kuwa, Palestina itakombolewa pale tu Wapalestina watakapoendelea kusimama kidete, kuendeleza muqawama na kutofumbia macho hata haki yao moja.

No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO