Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Iran amesema, lengo la kuwekwa makombora ya Jumuiya ya Kijeshi ya NATO nchini Uturuki ni kuulinda utawala wa Kizayuni wa Israel. Ramin Mehmanparast amesema hayo katika safari yake ya hivi karibuni nchini Uturuki ambapo maafisa wa nchi hiyo walimwambia kuwa, kuna uwezekano wa kutokea mashambulizi ya kijeshi kati ya Uturuki na Syria na kwamba makombora hayo yana lengo la kuisaidia Ankara iwapo itashambuliwa na Damascus. Mehmanparast hata hivyo amesema, Iran inaamini kuwa, nchi za Magharibi na NATO zimeweka makombora hayo nchini Uturuki ili kuuunga mkono utawala wa Kizayuni, iwapo utataka kuishambulia Iran. Pia Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema, Uturuki haipaswi kushiriki katika vita vyoyote vinavyoweza kuanzishwa dhidi ya Iran au kuruhusu anga yake kutumiwa dhidi ya Tehran.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO