Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetuma misaada ya kibinadamu kwa Waislamu wa kabila la Rohingya wa nchini Myanmar, huku jamii ya kimataifa ikiendelea kunyamaziwa kimya jinai wanaozendelea kutendewa Waislamu hao. Mahmoud Mozaffar Mkuu wa Jumuiya ya Uokoaji na Utoaji Misaada ya Kibinadamu ya Hilali Nyekundu ya Iran amesema kuwa, msaada huo ni wa tani 30 zinazojumisha vyakula, mahema, mablanketi na vifaa vingine muhimu. Ameongeza kuwa, ataongozana na timu yake kuelekea Myanmar kwa ndege na mizigo hiyo ili kusimamia ugawaji wa misaada hiyo ya kibinadamu kwa Waislamu wa Kirohingya na kushuhudia kwa karibu hali ya mambo nchini humo.
Karibu Waislamu 800,000 wa Mynamar wananyimwa haki zao kutokana na siasa za kibaguzi zinazotekelezwa na mabudha wa nchi hiyo huku wakitendewa jinai mbalimbali na kufukuzwa katika makazi yao.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO