Friday, April 12, 2013

KERRY AFANYA ZIARA KOREA YA KUSINI

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry amewasili Korea ya Kusini leo kwa mazungumzo na viongozi wa huko juu ya kuukwamua mzozo katika Rasi ya Korea. Kerry anatarajiwa kukutana na Rais Park Geun Hye na waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Korea ya Kusini, Yun Byung Se, katika ziara yake hiyo ya kwanza nchini humo kama waziri wa mambo ya nje. Maafisa wa Korea ya Kusini wamesema mazungumzo hayo yatajikita juu ya vitisho vya Korea ya Kaskazini dhidi ya Kusini na Marekani. Korea ya Kusini imesema iko tayari kufanya mazungumzo na majirani zao ili kutuliza hali ya taharuki ambayo imezidi tangu jaribio la tatu la kombora la Korea ya Kaskazini mwezi Februari mwaka huu. Rais Park aliwaambia wabunge wa chama tawala hapo jana kuwa ana nia ya kuanzisha mazungumzo na Kaskazini. Kerry atazizuru pia Japan na China katika ziara ya barani Asia inayoonekana kuimarisha uhusiano wa kiusalama na kibiashara na mataifa ya huko.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO