Wednesday, January 02, 2013

SUDAN KUSINI TUKO TAYARI KUONDOA MAJESHI MPAKANI

Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amesema kuwa nchi yake iko tayari kuondoa wanajeshi wake katika mpaka unaogombaniwa kati ya nchi hiyo na Sudan. Rais wa Sudan Kusini ameyatamka hayo katika hotuba yake ya kuukaribisha mwaka mpya  na kuongeza kuwa yeye na mwenzake wa Sudan Omar al Basher wamepanga kukutana baadae mwezi huu katika juhudi za kutafuta njia ya kuainisha eneo la mpaka ambalo litasimamiwa na wanajeshi wa nchi zote mbili na wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa. Amesema Juba imeamua kuondoa wanajeshi wake kwa muda katika eneo la mpaka lenye mzozo kati ya Sudan Kusini na Sudan ili kuweza kuanzisha kikosi cha wanajeshi watakaosimamia eneo hilo.  

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO